Header Ads

Header ADS

Majaliwa atoa onyo kwa Watendaji wa Kata na Askari.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewapa onyo Watendaji Kata na Polisi Nchini ambao wamekuwa hawazifikishi  sehemu husika kesi za uwapaji mimba wanafunzi na amesema kuwa kwa watakao bainika sheria kali itachukuliwa juu yao.
  Hayo amezungumza jana wakati akitoa hotuba kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika Wilayani kilolo katika uwanja wa ilula sokoni mkoani Iringa.















“Wanafunzi bado wanaendelea kupewa ujauzito na kukatishwa masomo yao huku watu waliohusika na vitendo hivyo wakishindwa kuchukuliwa hatua stahiki kwa sababu baadhi ya watendaji na askari wamezikalia kesi zao na kushindwa kuwafikisha polisi.”
   “Watoto wa kike lazima walindwe ili wamalize masomo yao waje kulitumikia Taifa lao, Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi.” Amesema Majaliwa.
     Waziri Mkuu alikagua Ujenzi wa mradi wa maji wa Ilula na kuweka jiwe la msingi,kabla ya kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.Pia alishughulikia ukarabati wa chuo cha maendeleo ya wananchi Ilula.

No comments

Powered by Blogger.