Header Ads

Header ADS

Raisi wa zamani wa Zimbabwe Robart Mugabe afariki dunia .

       Raisi wa kwanza wa Zimbabwe Robart Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 .Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na mmoja wa wanafamilia kuwa kiongozi huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.














     Mugabe alikuwa  nchini Singaporo akipata matibabu kwa kipindi cha muda mrefu .Pia kiongozi huyo ameiongoza Zimbabwe ktoka mwaka 1980 mpaka 2017 alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa kijeshi.
     Pia Rais ,wa sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kupitia ukurasa wake wa twita amethibitisha kutokea kwa kifo chake.
It is with the utmost sadness that I announce the passing on of Zimbabwe's founding father and former President, Cde Robert Mugabe (1/2)
Mugabe alizaliwa mwaka februari 21,1924 kwenye koloni la Rhodesia na alifugwa Jela kwa muda wa miaka 10  bila kufunguliwa mashitaka kwa kuukosoa uongozi wa Rhodesia mwaka 1964 .Mwaka 1973 wakati yupo Gerezani alichaguliwakuwa Rais, wa Chama cha Zimbabwe Union [ZANU] ambacho alikuwa ndiye mwanachama mwanjilishi  baada ya kuachiwa kutoka Gerezani alikimbilia Msumbiji na kuongoza mapambano ya Kijeshi ya kudai uhuru.
    Licha ya kuwa mpiganaji wa vita vya kushitukiza alisifika kwa kuwa mzuri kwenye majadiliano.Mwaka 1980 alifanikiwa kuingia madarakani baada ya uchaguzi uliomaliza utawala wa walowezi wachache wa kizungu.



No comments

Powered by Blogger.