Header Ads

Header ADS

Tanzania na Uganda za saini mkataba wa kuinuana kiuchumi

       Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uganda kwa pamoja zimetiliana sahihi hii leo hati za makubaliano ya kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo ,uhamiaji na magereza.













         Makubaliano hayo yamefanyika leo septemba 06 ,2019 Jijini Dare s Salaam katika kongamano la kwanza la biashara na uwekezaji ambapo Raisi wa Tanzania Dr Magufuli na Raisi wa Uganda Yoweri Mseveni wameshuhudia wakati wa utiaji wa saini hizo.Pia Waziri wa Mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa Afrika mashariki Palamagamba Kabudi wa Tanzania na Sam Katesa wa Uganda wameshudiwa wakisaini hati hizo
         Kwa mjibu wa kongamano hilo moja ya malengo makubwa ni kuunda jukwaa linalo wezesha kuruhusu sekta binafsi kutoka Tanzania na Uganda kushirikishana uzoefu ,kuunda mitandao ya kibiashara ,kubaini frusa na changamoto za biashara inayoendelea na uwekezaji na kuonyesha bidhaa na huduma yao kwenye maonyesho.
         Pia kongamano hilo ambalo nifrusa  muhimu sana katika nchi hizo mbili ya Tanzania na Uganda linaratibiwa na TPSF ,ambapokutakuwa na maonyesho biashara kuanzia leo 06 Septemba 2019 hadi 07 Septemba 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere uliopo Jijini Dare s Salaam.

No comments

Powered by Blogger.