Header Ads

Header ADS

Serikali yazuia Magari yenye kutu kubeba Nyama.

     Kwa mujibu wa bodi ya nyama nchini imepiga marufuku kwa magari yaliyo na kutu kubeba nyama hiyo ni kutokana na uhatari wa kutu kwa binaadam na hivyo kusema kuwa serikali haitopuuza kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kwenda kinyume na agizo hilo.
         Hayo amesema wakati akiwa jijini Arusha katika maonyesho ya teknolojia ya uchakataji nyama yaliyokutanisha wanachama cha wachinjaji pamoja na wafanya biashara wa nyama katika jiji hilo,Kaimu Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania, Imani Sichalwe amesema kuwa wamechukua hatua hiyo ili kulinda ubora wa nyama na kulinda afya za walaji  kwa kiuhakikisha kuwa magari yenye kutu hayataruhusiwa kubeba nyama pamoja na ubebaji wa nyama mgongoni.















  Alex Lasiki ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wachinjaji ameiomba Serikali kwa upande wa kutumia vigogo vya miti ya kukatia nyama na kuweka mashine ya kukatia nyama hilo ni kutokana na Wachinjaji  wengi kukabiliwa na tatizo la mitaji yao kuwa midogo ili waweze kujipanga kwa ajili ya mashine hizo za kisasa.
    Ismail Kulanga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha ameahidi kuwa Jiji la Arusha litashirikiana na machinjio ya Arusha meat kuhakikisha huduma bora zinatorewa pamoja na lengo la kuboresha mazingira ya machinjio hayo.

No comments

Powered by Blogger.