Header Ads

Header ADS

Asasi mbili za kiraia[ACHA na TRW] zinatarajia kupeleka waangalizi 215 katika wilaya zote Nchini.

 ASASI mbili za kiraia za Action for Change(ACHA) na The Right Way (TRW) zinatarajia kupeleka waangalizi jumla ya 215 katika Wilaya zote za Tanzania Bara kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu.
  Aidha imeelezwa  kuwa ACHA na TRW kwa pamoja wanadhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia na uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2019 sanjari na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ili kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru zaidi, za haki za kuaminika Nchini kote.
   Jackson kisahanga ofisa Mradi wa ACHA akizungumza leo jijini Dar es salaam kuhusu serikali za mitaa kwa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020 amesema wanatarajia kupeleka waangalizi hao kuhakikisha wanafuatilia mchakato mzima wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
      












 "ACHA TRW tuna matarajio kwamba uchaguzi huu utakuwa huru, haki , kuaminika , tulivu na wenye amani.Pia utakuwa wa uwazi na utakaoshirikisha makundi maalumu , mfano watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na wazee.

"Ni dhahiri kuwa uangalizi wa uchaguzi huu utafanyika pia kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa na mafunzo bora yatakayotolewa kwa wakati katika nyanja zote za michakato ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi,"amesema na kuongeza uangalizi na umakini huo katika utoaji taarifa vitabainisha maeneo yenye ucdhaifu kwa marekebisho kwa siku zijazo
  Aidha,  Sikahanga amesema ACHA na TRW zinalenga kuona mchakato wa uchaguzi unaofuata viwango vya kitaifa na kimataifa, kama ambavyo Tanzania imeridhia na zile zilizopo kwenye sheria za manispaa , kanuni na miongozo kutoka vyombo mbalimbali vya kusimamia uchaguzi ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
   Hata hivyo amesema kuwa, uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu mwaka 2020 ni fursa nyingine kwa Watanzania kushuhudia ukuaji wa utawala wa demokrasia. Aidha amesema ipo haja ya ushiriki mpana wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi, kaunzia kipindi kabla ya uchaguzi kwa mfano uandikishaji  wa wapiga kura, elimu ya mpiga kura na uteuzi katika vyama vya kisiasa
    ."Mchakato huu unahitaji mfumo wa mwenendo thabiti wa elimu kwa wananchi katika zoezi zima, ambalo litafanya elimu kwa mpiga kura kuwa thabiti na wenye tija , mwamko huu wa wananchi kupitia elimu kwa umma na programu ya mpiga kura , ambayo imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwadaidia wananchi kutambua kuwa ushiriki katika uchaguzi ni haki yao,"ameeleza.   Pia, kwa upande wake Mkurugenzi wa TRW Rhoda Kamungu amesema upo ushahidi usiojitosheleza unaunga mkono umuhimu wa vyombo katika kuhakikisha Serikali inawajibika juu ya utawala bora ,haki na misingi yote ya haki za binadamu na kwa wananchi wake.
  "Ni jukumu letu kuwajulisha wananchi kama nguzo muhimu kupitia vyombo vya habari katika kutoa jukwaa jumuishi la mjadala wa umma na majadiliano kuhusu kuhamasisha mijadala kwa kuzingatia Katiba,sheria,sera ,taratibu na miongozo.Utafiti unadhihirisha kuwepo idadi kubwa ya wapiga kura wasiofahamu kuhusu mchakato na utaratibu wa uchaguzi,"amesema.
  Hata hivyo,  Kuhusu  elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura na ungalizi ni muhimu, Kamungu amejibu kuwa ACHA na TRW kwa pamoja wanatamani kuona mchakato wa uchaguzi ambao unaongozwa na wananchi, shirikishi , wenye uwazi , huru na haki. "ACHA na TRW tutatoa elimu ya uraia, mpiga kura na uangalizi wa michakato ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo.

No comments

Powered by Blogger.