Header Ads

Header ADS

Biteko Awataka Mawakala Wa Miundombinu Kuongeza Kasi Ya Utendaji Kazi

 Doto Biteko (CCM) ambaye Mbunge wa Jimbo La Bukombe Mkoani Geita na Waziri wa Madini ameomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuongeza kasi ya uboreshaji miundombinu ya barabara jimboni humo ili kuvutia wawekezaji zaidi.

  













 Aidha Biteko ametoa ombi hilo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Geita ambacho pamoja na mambo mengine kimejadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara.
   Amesema wakati Serikali inaendelea kuboresha mapori yaliyopo wilayani Bukombe kuwa na hadhi ya kuvutia watalii, ubora wa miundombinu ya barabara utavutia zaidi wawekezaji hivyo mamlaka hizo ni vyema zikatekeleza miundombinu iliyokwisha ingiza kwenye mpango.
  Pia  Naye Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
ameshauri mamlaka hizo ikiwemo TARURA kuzingatia vipaumbele vya wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge zinapokuwa zinatekeleza miradi ya barabara ili kuweza kukamilisha Miradi hiyo kwa haraka.

No comments

Powered by Blogger.