Header Ads

Header ADS

Lugola Afanya Mazungumzo Na Balozi Wa Ethiopia

Kangi Lugola ambaye ni Waziri Wa Mambo Ya Nje  amefanya mazungumzo na Balozi wa Ethipia Yonas Yosef Nsabe Hapa Nchini  kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
  Hata hivyo  Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma, leo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na Ethiopia.

     











Lugola alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini hapa.
  "Mheshimiwa Balozi Nashukuru sana kwa kunutembelea,najisikia furaha kwa ujio wako karibu sana na wakati wowote Wizara pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali"alisema Lugola
   Lakini Kwa upande wake Balozi Sanbe, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Ethiopia na Tanzania.
  NA MWANDISHI WETU, DIANA MALEKELA
   

No comments

Powered by Blogger.