Header Ads

Header ADS

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) chakanusha kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) chakanusha kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kama ambavyo barua kutoka kwa msajili wa Vyama vya Siasa nchini inavyoeleza.

 









Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Wa Chama hicho Tumaini Makene ,hata hivyo chama kimekiri kupokea taarifa hiyo lakini wamesema Katiba ya Chama hicho inatoa mamlaka kwa Kamati kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama.
   ” Tarehe ya uchaguzi mkuu wa chama, inaweza kurekabishwa kwa kusogezwa mbele kwa muda usiozidi mwaka mmoja, toka mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo, mamlaka ya kufanya marekebisho haya yameachwa kwa kamati kuu” imeeleza taarifa hiyo.
  Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hiyo,Kamati kuu ya Chama hicho ilikaa katika kikao chake cha tarehe 27 na 28 julai 2019 na kurekebisha ratiba ya uchaguzi, ambapo utakamilika mwezi Disemba kwa ngazi ya taifa na kwamba kwasasa kinaifanyia kazi barua hiyo ili iweze kuifikia Ofisi ya msajili wa vyama vya Siasa ndani ya muda husika.
   Aidha awali Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini ilitoa taarifa kuwa Uongozi wa Chama hicho Chini ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe umemaliza muda wake tangu Septemba 14,2019 na kukitaka kuandika maelezo ya kwanini kisichukuliwe hatua baada ya kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na kuwataka kuwasilisha maelezo hayo  Oktoba 07 mwaka huu,majira ya saa 09:30 jioni.

No comments

Powered by Blogger.