Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli ampongeza Chalamila kwa kuwatandika fimbo wanafunzi wa Chunya

Rais John Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kwa kuwachapa viboko wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita wa shule ya Sekondari Kiwanja Wilayani Chunya kwa madai ya kuhusika na kuchoma mabweni mawili ya shule hiyo.
   ''Leo nilikuwa naongea na mkuu wa mkoa wa Mbeya nikamwambia nakupongeza sana kwa kuwatandika wale viboko na nikawaambia uliwatandika viboko vichachee...haiwezekani serikali tunatoa mabilioni kwa ajili ya kujenga madarasa na shule halafu mtoto anaenda kuichoma''. Alisema rais Magufuli.











Hata hivi  Rais huyo ambaye yuko ziarani eneo la nyanda za juu kusini alimwambia Chalamila kuwa watoto wote ambao walihusika na vitendo hivyo wafukuzwe shule.
   ''Nikamwambia watoto hao wote fukuza wote, kwa hiyo watoto wote wamefukuzwa, na bodi imevunjwa kwasababu ile pia uzembe wa bodi ya shule hiyo..eti haki za binadamu, haki za binadamu watoto wawe na viburi vya kipumbavu hivyo. Ni lazima tuache mchezo katika maendeleo'', alisema.
  Na ameongeza kuwa wazazi wa watoto hao wanapaswa kulipa gharama za majengo yaliyoharibiwa.
 ''Nafikiri kama mahali tulikosea ile sheria ikafanyiwa marekebisho wawe wanatandikwa viboko... Ati mkuu wa mkoa alitandikwa viboko hata Ulaya wanatandika viboko...Kiboko kinafundisha''
  Hata hivyo mpaka sasa tayari wanafunzi hao wameshafukuzwa shule na kupigwa faini,na pia awali Chalamila alikosolewa na Waziri wa Serikali za Mitaa Sulemani Jafo kwa kitendo cha kuwapiga wanafunzi kwa madai kuwa hana mamlaka akisema kuwa hamna Sheria inayomruhusu  Mkuu wa Mkoa kuwaadhibu wanafunzi.
    Lakini hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alijijitetea kwa kusema yeye ni Mkuu wa Mwalimu Mkuu na anawajibu wa kufanya kitendi hicho.,
Video hizo zilionyesha kikundi cha wanafunzi wakiwa wamelala chini huku nyuso zao zikitazama ardhini wakati Bwana Chalamila akiwatandika viboko vitatu vitatu kila mmoja, huku wanafunzi wengine wakitazama.
     

No comments

Powered by Blogger.