Rais atatua mgogoro wa ardhi Songwe
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewaqaqgiza wakazi wa Nanyala wilayani Mbozi moani Songwe kuendelea kutumia eneo lenye ukubwa wa hekari 2,115 linalogombaniwa baina ya wakazi hao na kiwanda cha saruji mbeya.
Ametoa maagizo hayo wakati wa Ziara yake katika kijiji hicho mkoani Songwe wakati Philemon Namwema Mwenyekiti wa kijiji hicho alipokuwa akimueleza kero hizo.
Namwema amesema kuwa mgogoro huo umedumu kwa kipindi cha mda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli nyingine yoyote huku wananchi wengine 23 wakikabiliwa na kesi mahakamani.
Aidha Rais Magufuli amewaagiza Mawaziri husika kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo na baada ya hapo watatakiwa kumjulisha Rais ili aweze kubadili matumizi ya ardhi katika maeneo hayo.

No comments
Post a Comment