Header Ads

Header ADS

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya awafukuza wanafunzi wa kidato cha 5 na cha 6 katika shule ya Sekondari Kiwanjani.

   Albert Chalamila ambae ni mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewafukuza wanfunzi wa kidato cha 5 na cha 6 kwa kosa la kuchoma Mabweni mawili moto, lakini pia amewapa likizo walimu wa kidato cha 5 na 6 katika Sekondari hiyo ya Kiwanjani iliyopo wilaya ya Chunya Mkoani mbeya
     Ambapo amewataka wanafunzi hao kurejea shuleni Oktoba 18,2019 na kila mwanafunzi akiwa na kiasi cha fedha shiling laki mbili (200,000) kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo.










''Nimechukua hatua hiyo kwa sababu ndiyo wanayostahili,nimewafukuza wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita warudi kwa baba zao,na kama wanawaza kuchoma majumba wakachome za babu wao,na sio waje wachome majengo ya Serikali ambayo yamejengwa kwa jasho la Watanzania,kodi za watanzania ,fedha za Mh.Rais hatuwezi fuga upumbavu wa namna hii kwa mkoa wa mbeya kwahiyo warudi kwa wazazi wao waende wakachukue fedha laki mbili mbili za kuja kujenga mabweni kunyume na hapo watafungwa.''Amesema Chalamila
    Lakini kwa upande wa asasi za kiraia na za kisheria zimekinzana na maamuzi ya mkuu wa Mkoa wa mbeya,kupitia mwanasheria Amani Angolwise amezungumzia suala hilo la Mkuu wa mkoa kuwacharaza wanafunzi viboko,ambapo amesema''Kwanza tukubaliane na jambo hilo la kuungua Majengo wote kama watanzania na wanasheria hatukubaliani na jambo hilo,pili sisi kama watanzania na viongozi tuheshimu na kufuata sheria,tunafahamu kwamba mtu yeyote akifanya kosa hawezi kuadhubiwa labda tu mahakama imetoa amri hiyo bila kujali mwanafunzi au si mwanafunzi,kuna vyombo ambavyo vipo kisheria kwa ajili ya upelelezi na wahusika hupelekwa mahakamani,katika nchi yetu kuna kanuni za adhabu mashuleni kanunu hizo hakuna sehemu ambazo zina mruhusu mtu baki ambaye si mwalimu kumwadhibu mwanafunzi,kwahiyo kitendo alichokifanya mkuu wa mkoa wa Mbeya hapo jana amekiuka taratibu na sheria.''ameeleza mwanasheria huyo.
  Imeandaliwa na Repota Adolf Mwingira kutoka Mbeya.
    

No comments

Powered by Blogger.