Header Ads

Header ADS

Dkt.Angeline Mabula akataza utoaji vibali vya ujenzi wa viwanda maeneo ya makazi ya watu.

  Katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Dkt.Angeline Mabula ambaye ni waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi amepiga marufuku utoaji wa vibali vya ujenzi wa viwanda katika maeneo ya makazi ya watu.
   Hayo amezungumza hapo jana wakati amekutana na uongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati wa kutatua migogoro ya ardhi lakini pia katika uhamasishaji wa ukusanyaji mapato ya Serikali kupitia kodi ya ardhi.
   Aidha,Dkt.Mabula ameeleza kuwa  halmashauri ya wilaya ya Mkuranga lazima iandae Mpango Kabambe ambao utakuwa dira ya halmashauri hiyo kuonesha matumizi ya ardhi yake kwa kuwa maeneo kama viwanda, makazi na matumizi mengine yatakuwa yameoneshwa na kuondoa ujenzi wa makazi holela.











   ‘’Mkuranga lazima iwe na mpango wa matumizi ya ardhi unaoonesha viwanda vikae wapi, siyo viwanda kujengwa kila kona na katika mipango yenu halmashauri muandae maeneo yatakayowekwa viwanda’’ alisema Dkt Mabula.
  Lakini pia,Dkt.Mabula amesema kuhusu zoezi la ulasimishaji ameitaka Wilaya hiyo kuharakisha zoezi hilo ili kuepuka makazi holela na kubainisha ucheleweshaji wowote utasababisha mji kutopangika na kusisitiza zoezi hilo lazima lisimamiwe kwa umakini.
     Aidh,ameeleza katika upande wa upimaji maeneo katika wilaya ya Mkuranga pamoja na kuwa inaviwanda vingi lakini haijaweza kufanikiwa katika zoezi hilo na kushauri katika zoezi hilo la upimaji Halmashauri lazima maeneno ya uwekezaji yatengwe.
   Kwa upande wake Abdallah Ulega ambaye ni  Mbunge wa jimbo la Mkuranga lakini pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi alisema, wilaya ya Mkuranga ina viwanda vingi kutokana kuwa na eneo linalovutia na kuongeza kuwa atafurahi kama Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itafanya jitihada za kuharakisha zoezi la urasimishaji.
     ‘’Kama serikali itaongeza kasi kidogo ya kupanga na kurasimisha maeneo ya wilaya hii basi itakusanya kiasi kikubwa cha fedha maana Mkuranga imekuwa lango la ni kimbilio la wananchi kutoka Dar es Salaam kutokana na mkoa huo kujaa na mahali pekee pa kupumulia ni Mkuranga’’ alisema Ulega
  Hata hivyo,mhandisi Mshamu Munde ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga alimwambia Naibu Waziri wa Ardhi kuwa halmashauri yake ina migogoro mingi ya adhi ya kurithi na katika kukabiliana changamoto za ardhi ikiwemo makazi holela, tayari kuna Kampuni saba zinazofanya kazi ya urasimishaji na kusisitiza kuwa mkakati wa halmashauri yake ni kuzuia uanzishwaji makazi holela.
    Philberto Sanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mkuranga,katika hatua nyingine amemtaka Welbert Mduma ambaye ni mtumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya hiyo kujisalimisha mara moja kujibu tuhuma inayo mkabili ya uhujumu mradi wa upimaji viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Mkuranga katika maeneo ya Kikoo na Miale.
    Aidha,Mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa mtumishi huyo muda mrefu hajaonekana katika Ofisi za halmashauri ya Mkuranga ambapo tokea awasili akitokea Morogoro alipohamishiwa mara tu baada ya kufanya 'Madudu' katika mradi wa fidia ya ardhi.

No comments

Powered by Blogger.