Header Ads

Header ADS

Simu kuanza kutumika kwa wafugaji Kufuata maji na malisho.

   Katika Mkoa wa Arusha wilaya tatu ambazo wafugaji watakuwa wanatumia ujumbe za simu kwa ajili ya kupata maelekezeo sehemu ambayo wanaweza kupata maji pamoja mna malisho kwa ajili ya mifugo yao.
     Shirika la kimataifa PCI,L, limezindua mradi huo katika kijiji cha Arkalia Wilayani Monduli lakini pia katika wilaya ya Ngorongoro na Langido wilaya ambazo zina mifugo mingi pia mradi huo utatekelezwa.















 Rais wa PCI,ambae ni Carrie Hetessler Raadelet akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema wafugaji hao kupitia simu zao za mkononi mara tu baada ya kuwa na aplication ya Afriscout watatuma ujumbe kwenda 15054 kuulizia maji na malisho pasipo kutozwa gharama yeyote.
    Aidha, Rais huyo amesema kuwa baada ya kuuliza mtandao huo utaunyesha ramani ya sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.
   Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli zingine za kiuchumi.
    Lakini pia, Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.“tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisema.
        Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi endeshji wa malisho na vyakula vya mifugo,Dk Asimwe Rwiguza alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.
   Hata hivyo,akizungumza mfugaji John Laezer ameeleza kwamba kutokana na mradi huo kwao itaondoa tatizo la mifugo kufariki majira ya kiangazi lakini pia migogoro dhidi ya wakulima.Lakini kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli ambaye ni Joseph Rutabingwa ameeleza kuwa Halmashauri ya Mondule itatoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huo ili wafugaji waweze kunufaika zaidi.
     Aidha,katika nchi tatu barani mradi huo unatekelezwa ambazo ni Tanzania,Ethiopia pamoja na Kenya hata hivyo katika nchi 16 duniani ambazo shirika hilo linafanya kazi.
     Mwandishi wetu;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.