Header Ads

Header ADS

Dkt.Angeline Mabula ameomba kupatiwa Majina ya watumishi walioshindwa kuhamia Mafia.

         Dkt.Angeline Mabula ambae ni Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ametaka kupatiwa majina saba ya watumishi wa sekta ya Ardhi ambao wameshindwa kuripoti katika kituo chao kipya cha kazi ambapo walipangiwa kuhamia Halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani.
        Ametoa agizo ilo jana akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani pwani katika wilaya ya Mafia akihamasisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia kodi ya ardhi,Akikagua mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektroniki, pia kukagua Masijala ya ardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi.













        Aidha, Kauli ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia kuelezwa na Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma kuwa wilaya yake ina mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi jambo linaloifanya wilaya hiyo kushindwa kutekeleza majukumu ya sekta hiyo ipasavyo.
      Pia, Naibu  waziri mabula alisema kuwa wizara yake italifanyia kazi suala hilo mapema kwa kuwa ni vigumu wilaya kufanya kazi vizuri katika sekta ya ardhi kwa kutegemea mtumishi mmoja hasa ikizingatiwa sekta hiyo inahitaji kuwa na wapimaji, wathamini pamoja na wataalamu wa mipango miji. 
      
‘’Mafia mna mtumishi mmoja wa sekta ya ardhi? Suala hili inabidi lifanyiwe kazi mapema na wizara yangu italifanyia kazi kuhakikisha wilaya inakuwa na watumishi wa njanja zote katika sekta ya ardhi’’ alisema Dkt Mabula
      Mwanzo mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alimweleza naibu waziri changamoto kubwa inayo ikabili wilaya yake kwa upande wa sekta ya ardhi kutokuwepo kwa watumishi wa kutosha hali ya kuwa wilaya hiyo imekua na mtumishi mmja  kwa kipindi cha muda mrefu baada ya mtumishi mwingine wa uthamini kupangiwa majukumu katika sekta nyingine.
     Aidha,mkuu wa wilaya amesema kuwa licha ya kufwatilia upatikanaji wa watumishi wa sekta hiyo zimeonekana kukwama kwa kuwa hadi sasa hawajapata watumishi wengine hali hiyo imesababisha wilaya kushindwa kutekeleza majukumu yake.
      ‘’Watumishi saba walipangiwa kuja Mafia lakini wameshindwa kuripoti na hapa unavyotuona tuna mtumishi mmoja, hatuna wataalamu kama wangekuwepo wangesaidia upangaji. Wilaya ni kama imesimama katika sekta ya ardhi’’ alisema Nnunduma
       Kwamujibu wa Nnunduma ameeleza kuwa, kufika kwa Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo katika wilaya yake unaweza kuleta mafanikio kwa kupata watumishi kwani tangu alipoteuliwa na Rais kuwa mkuu wa wilaya hiyo ndiyo anashuhudia Waziri wa kwanza wa sekta ya ardhi kutembelea wilaya hiyo kama  itatumiwa vizuri kupitia sekta ya utalii itawezesha serikali kukusanya mapato mengi katika wilaya hiyo.
      Lakini pia Mubaraka Dau ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, alimueleza Dkt.Mabula kuwa ingawa kuna changamoto nyingine lakini wilaya hiyo inakabiliwa tatizo kubwa la kutokuwepo kwa  baraza la ardhi la wilaya kutokuwepo kwa baraza hilo linawalazimu kufunga safari hadi baraza la Mkuranga hili hiyo inawafanya wananchi kushindwa kufuatilia haki zao za ardhi.
      Mwandishi ;Fatma Maulid.

No comments

Powered by Blogger.