Header Ads

Header ADS

Waziri Jafo atoa agizo kwa wakuu wa shule za msingi.

   Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)amewataka wakuu wa shule za msingi zote kutojihusisha na suala la udanganyifu wa mitihani kwa sababu hali hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kudumaa kwa elimu nchini.









    Hayo amezungumza hapo jana wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu, wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara akiwa jijini Dodoma.
    Aidha,Jafo amesema kwamba wao wanadhamana kubwa katika kusimamia sekta ya elimu nchini hivyo ikitokea uvujaji wa mitihani hauleti picha nzuri katika Taifa.
        Hata hivyo,Waziri Jafo ameeleza kuhusu suala la elimu bila ya malipo amesema matumizi ya fedha hizo yameimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo walipoanza ambapo kulijitokeza changamoto mbalimbali.
  Lakini pia kwa upande wake Rehema Ramole ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha),ametoa pongezi kwa Serikali kwa kuboresha miundombinu jambo ambalo limepelekea kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani kwa kiasi kikubwa sana.
    Uwajibikaji na usimamizi makini wa Raslimali katika elimu ndio msingi wa Elimu Bora,hii ndiyo kauli mbiu ya mkutano huo.
          Mwandishi;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.