Erick Kabendera ataka kujadiliana na DPP namna ya kumaliza kesi inayomkabili.
Wakili wa mwandishi wa habari nchini Tanzania ambae ni Jebra Kambole,ni wakili wa Erick Kambendera ameieleza Mahakama ya mkazi Kisutu kwamba mteja wake anaitaji kuongea na Mkurugenzi wa mashtaka(DPP) ili kuangalia jinsi gani watamaliza kesi yake inayomkabili.
Hayo amezungumza mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Augustine Rwizile huku wakili wa Serikali, Wankyo Simon akiieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika.
Aidha, Kambole ameijulisha mahakama taarifa kuhusu Kabendera kujadiliana na DPP kwamba ni kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019,Baada ya Wankyo kueleza hayo.
Kwa mujibu wa majibu aliyotoa Wankyo amesema jambo hilo ni kweli na wapo katika mchakato, akisisitiza kuwa taratibu zikikamilika wataipa taarifa mahakama.
Aidha,Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh173 milioni.
Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Lakini pia,mnamo januari 2015 na julai 2019 katika shitka la utakatishaji fedha anadaiwa alijipatia sh.173.24 milioni lakini alitambua wazi wakati anazipokea fedha hizo ni mazao ya makosa yaliyotangulia ya kujihusisha ka genge la uhalifu pamoja na ukwepaji ulipaji kodi.
Imeripotiwa na mwandishi wako; Adolf Mwingira
No comments
Post a Comment