Header Ads

Header ADS

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Amewataka VIjana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi.

    Omary Mwanga  ambaye  ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi [UVCCM]  Mkoa wa tanga amewataka Vijana kujitokeza kwa wingi kuwania  nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Uchaguzi  wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji.
    Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake ya utekelezaji ya [UVCCM] mkoa wa Tanga kaika Wilaya ya Kilindi na Handeni iliyojumuisha Mjumbe wa baraza kuu la [UVCCM] mkoa Mbarouk Asilia na  katibu wa [UVCCM ] Mkoa huo Zawadi Nyambo.










   Aidha,amesema kuwa malengo ya ziara hiyo ni kuhamasisha vijana wanashiriki kikamilifu,kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,na vijiji na vitongoji ambao hutafanyika mwaka huu.
   Pia Mwenyekita huyo pili ni kusisitiza vijana kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 ikiwemo kukagua uhai wa jumuiya ngazi ya Kata ambapo ziara hiyo ilihusisha kata za segera, kabuku, mkata, mabanda, mdoe, chanika, jaila na mabalanga.
    Hata hivyo viongozi hao wa kimkoa waliwahamasisha vijana kugombea nafasi za uongozi katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji vyao kwenye uchaguzi huo.

No comments

Powered by Blogger.