Longido Yaweka Mikakati Itayowawezesha Kukusanya Bilion 100 Kwa Mwaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Wakili Juma Mhina amesema kuwa wilaya hiyo imepanga kukusanya bilioni 100 kwa mwaka zitazotokana na miradi ya kimkakati ambayo halmashauri hiyo imepanga kuitekeleza ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha nyama,ujenzi wa bwawa kubwa la kitalii na stendi ya mabasi.
Aidha Wakili Juma Mhina ameeleza kuwa ,wanatarajia kuanzisha miradi ya kimkakati Wilayani hapo, ambayo inahitaji Tsh billion 50, baadhi ya miradi taratibu zake zimeshakamilika.Wanatarajia kufanya mradi wa Nyuki,Maegesho ya magari makubwa,ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama cha serikali,Soko la Mazao la kimataifa na Dampo la kisasa.
Hayo ameyasema Akizungumza katika kikao maalumu cha Watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo ,Mkurugenzi hiyo amesema kuwa wilaya hiyo ina miradi ya kimkakati ambayo inatafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji ambayo ikikamlika itaifanya Longido kuwa Wilaya inayoongoza kwa kukusanya mapato nchini .
Fidelis Raphaeli ambaye ni mweka hazina wa halmashauri hiyo amesema kuwa watumishi wa halmashauri wana nafasi kubwa katika kushiriki kuisaidia halmashauri kutimiza malengo take ikiwemo kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake, Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo Steven Mbombe amesema kuwa serikali imefanya vizuri katika miradi ya maendeleo hivyo kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kutasaidia kuinua uchumi.
No comments
Post a Comment