Header Ads

Header ADS

Mkuu Wa Wilaya Bukoba Atoa Onyo Kwa Wauguzi Wa Afya

Bw.Deodatus Kinawilo Ambaye Ni Mkuu wa wilaya Bukoba,  amewataka wahudu wa Afya mkoani humo kwenda kutekeleza zoezi la chanjo ya surua lubera na chanjo ya polio sindano kikamilifu ili kufanikishwa malengo ya mkoa katika zoezi hilo la Utoaji Chanjo.













Hayo ameyasema  katika ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya wahudumu wa afya watakao kwenda kutekeleza zoezi la chanjo ya Surua lubera na chanjo ya polio sindano katika jamii kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kagera Brig. Jen. Marco E Gaguti.
  Aidha wakati Akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa Kagera DC Kinawilo amesema kuwa mkoa Kagera unalenga kuwafikia watoto wapatao 486, 675 kwa ajiri ya chanjo ya surua lubera na watoto 228, 066 kwa ajiri ya chanjo ya polio sindano ambapo chanjo hizi zitatolewa kwa watoto walio na umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka mitano hayo ndiyo Malengo waliyoyaweka.
   "Mwaka 1990 vifo vya watoto kitaifa vilikuwa 191 kwa vizazi hai 1000 kwa lengo la nne la milenia tulilenga kupunguza vifo hivi hadi 40 kwa vizazi hai 1000 ifikapo 2020 tunajivunia kuwa hata kabla ya kufika 2020 mkoa wetu wa Kagera tayati tumepunguza vifo hivyo kufikia vifo 7 kwa vizazi hai 1000 hadi kufikia 2018, lakini sisi kama mkoa tunasema hata hivyo vifo vya kila vizazi 1000 ni vingi tunapenda vipungue au ikiwezekana viishe kabisa" DC Kinawilo asema.
  Pia Chanjo ya surua lubera na polio sindano zitatolewa bure kwa wananchi wote ambapo DC Kinawlio amesema kuwa hategemei kusikia minong'ono ya aina yoyote kutoka kwa wananchi kuwa wanatozwa pesa kwa ajiri ya Chanjo hiyo hivyo itatolewa bure.
   "Nisisitize mambo mawili hapa la kwanza hakuna mahala ambapo ni patata kama sehemu panapotumia fedha, ndugu zangu mnaoshika hii pesa hii, hakikisha mnashiriki kikamilifu katika kuhakikisha mnatumia pesa hii kwa malengo yaliyokusudiwa ili zoezi lifanikiwe na hili bila kumung'unya maneno swala la matumizi ya fedha kwa serikali ya awamu ya tano ni swala nyeti sana tunataka fedha zitumike kwa usahihi na kiuadilifu na tukisikia kuna mahali tumeokoa okoa fedha uwa tunafurai sana kuliko kusikia fedha zimekwisha na zoezi halikufanikiniwa hata asilimia 50% na mnataka fedha nyingine hapo patachimbika" Amesema DC Kinawilo.
    Vile vile Amewataka wahudumu wa afya kwenda kutekeleza zoezi hilo kwa uadilifu na kwa kujituma kwani serikali imewaamini na kuwapa majukumu ya kwenda kutekeleza zoezi hilo kwa weledi wa hali ya juu na haitakuwa vema kutekeleza zoezi hilo chini ya kiwango tofauti na malengo ya mkoa uliojiwekea ambapo amewataka kujitoa na kufanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa.
  Hata hivyo DC Kinawilo amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha pindi zoezi hilo litakapo anza kutolea katika maeneo yao ambapo zoezi hilo litaanza October 17 mpaka October 21/209 Yaani Mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.