Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Yatoa Pikipiki Kwa Watumishi Wa Vijijini Wa Halmashauri hiyo
Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe imefanikiwa kununua piki piki kumi na saba kwa kutumia mapato yake ya ndani na kugawa kwa watumishi wa halmashauri hiyo wanaohudumia maeneo ya vijijini kutokana na ukubwa wa maeneo yao ya kazi ili ziweze kurahisisha kazi zao.
Aidha,Akizungumza kabla ya kukabidhi piki piki hizo,mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminatha Mwenda,amesema wamechukuwa uamuzi huo ili kuweza kuwasaidia watumishi wenye maeneo makubwa ya kazi na kuendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.
“Kila pikipiki tumenunua kwa shilingi milioni mbili laki tano na themanini,na piki piki hizi kumi na saba tunawapa wafanyakazi wa vijijini ambao wana maeneo makubwa sana ya kufanya kazi,na utaratibu wetu ni kwamba asilimia 50% itabidi walipe na asilimie 50% nyingine itakuwa ni motisha kwa ajili ya kufanya kazi”alisema Iluminatha Mwenda.
Hata hivyo, Miongoni mwa watumishi waliopata usafiri huo ni pamoja na Yunis Mgaya kutoka idara ya kilimo kata ya Ramadhani anasema anafanya kazi na mitaa tisa hivyo alikuwa akipata wakati mgumu kuwafikia kwa wakati wakulima wa kata yake,lakini kwa upande wake Agustino Ngailo ambaye ni afisa mtendaji kata ya mji mwema amesema alikuwa anapata adha kubwa kufikia miradi mbali mbali ndani ya kata yake hivyo usafiri huo utasaidia kuifikia miradi kwa wakati

No comments
Post a Comment