TANROADS Yazindua Rasmi Ujenzi Wa Barabara Za Mzunguko Dodoma
Serikali kupitia Wakala wa barabara Nchini(TANROADS) leo imezindua rasmi ujenzi wa barabara za mzunguko (mchepuko) za njia nne Jijini Dodoma zenye urefu wa kilomita 112.3, ambazo ujenzi wake unagharimu kiasi cha sh.billion 494.
Aidha,Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuanza Ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo Afrika, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwele amesema huo ni mipango mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katikati ya jijini la Dodoma.
Pia,Amesema barabara hiyo ni kubwa na ni barabara kuu inayotoka Capetown hadi Cairo nchini Misri, hivyo katika kukabiliana na msongamano mkubwa wa magari wameamua kujenga barabara hizo kuepusha mlundikano wa magari Yasiyo na ulazima wa kuingia katikati ya Jiji.
Amesema mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 494 ambapo Benki ya Maendeleo Afrika imetoa shilingi billion 412 ambapo ni sawa na asilimia 83.4,huku serikali ya Tanzania ikitoa shilingi bilioni 82 sawa na asilimia 16.6 za mradi huo.
"Katika mradi huu banki ya Maendeleo Afrika imetoa zaidi ya shilingi bilioni mia nne(Bilioni 400) na Serikali itatoa Bilioni 82, pamoja na kulipa fidia halali kwa wananchi watakaopitiwa na ujenzi wa mradi huo hivyo tutalipa kwa wananchi ambao serikali ya Mtaa inamtambua," amesema Waziri Kamwelwe.
Aidha ameipongeza Banki ya Maendeleo Afrika kwa kuendelea kuiamini serikali na kutoa mikopo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania katika kuijenga nchi kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.
Lakini,Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara nchini (TANROADS)Mhandisi Patrick Mfugale amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa sababu kutakuwa na miradi mingine midogomidogo, ambapo watajenga vituo vya afya vitano katika vijiji vya Mahomanyika,Vyeyula,Nala,Ihumwa pamoja na Matumburu, ikiwemo na kununua magari ya kubebea wagongwa.
Hata hivyo,Mfugale amesema kupitia miradi huo watakarabati barabara chache za jiji ambazo ni kilomita 28.3 ambazo ni kutoka kizota hadi zuzu, mbali na hilo amesema wapo katika mkakati wa kuhakikisha wanazipanua barabara takiribani kilomita 15 kila upande kwa barabara zinazoingia katika jiji la Dodoma.
Pia, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge, wakati wa uzinduzi huo amesema barabara hizo zitakuwa mkombozi kwa wakazi wa Dodoma na itakuwa ni fulsa kwa vijana kupata kipato wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
No comments
Post a Comment