Header Ads

Header ADS

Hukumu ya Mbunge Sugu Yatenguliwa

        Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi maarufu kama ''Sugu'' Mahakama kuu kanda ya mbeya imetengua hukumu,Mwenendo na Kifungu alichohukumiwa Mbunge huyo,Kwa kusema kuwa ni kutokana na ubatili wa mwenendo wa kesi hiyo.
        Naibu Msajili wa Mahakama kanda ya Mbeya   Jaji Utamwa ndiy,e  isoma hukumu hiyo,Ameeleza kuwa hakubaliani na hoja za  upande wa Serikali ambao ndio wajibu rufaa.


       Aidha Jaji Utumwa ameeleza kuwa, kulikuwa na makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo, hasa pale aliyekuwa Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya aliposhindwa kuwasomea mashtaka washtakiwa katika hatua za awali.
     Hata hivyo,amesema kuwa madhaifu hayo,yaliathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga pia ametengua hukumu yao.                                 
    Aidha Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela katika kesi hiyo alitumikia miezi minne jela na kutoka kwa msamaha wa Rais mnamo Aprili 26,2018 katika maadhimisho ya miaka 58 ya muungano.
   Ikumbukwe kuwa mwezi Februari mwaka huu,Mheshimiwa Joseph Mbilinyi na katibu wa CHADEMA kanda ya nyanda za juu kusini,Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano na Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya.                                    
    

No comments

Powered by Blogger.