Header Ads

Header ADS

Kiongozi wa Chama cha ACT awataka wanachama kuonesha Demokrasia yao.

    Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo amewataka wanachama wote wa chama hicho kushikamana pia kuonesha juhudi na Demokrasia ya kweli kwa kushiriki chaguzi za kuchagua viongozi kuanzia ngazi za chini hadi mikoa.
    Hayo amezungumza akiwa katika Ofisi ya Chama  iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar,wakati akitoa tarifa ya kuanza kwa chaguzi hizo za chama ndani ya chama zinazotarajiwa kuanza ctoba 12 mwaka huu.
   Aidha,Zitto alisema ni lazma Demokrasia iliyoota mizizi ionekane namna inavyotekelezwa ndani ya chama hicho.















   “Ni lazma tuonyeshe ni namna gani demokrasia imeota mizizi na namna gani demokrasia inavyotekelezwa ndani ya chama chetu “alisema Zitto.

Wakati akitoa tarifa hiyo  alisema chaguzi hizo zitafanyika katika Mikoa mitano yenye  majimbo  54 ya Zanzibar.ikiwa ni 18 ya Kisiwani Pemba na 34 ya kisiwa cha Unguja, Wodi 111 na Matawi 679.

Hata hivyo alitoa wito kwa wanachama kushirikiana kikamilifu katika ngazi zote za chama kwani viongozi watakaochaguliwa ndio watakaopambana  katika chaguzi zijazo.

“Ni wajibu wa mwanachama kuchagua viongozi mahiri,wadilifu watakaohakikisha wanajenga mshikamano mzuri ndani ya chama utakaorahisisha ushindi katika uchaguzi mkuu”alisema Zito.

Aidha amewataka wagombe wote kuomba kura kwa njia ya kidemokrasia na kuepuka ulaghai,ufisadi katika mchakato wa uchaguzi ili baadae kuwa timu moja kwa wagombea wote aliyeshindwa na aliyeshinda.

“wote kwa pamoja watakuwa na wajibu wa kupambana na CCM kwani ni dhahir chama cha ACT ni chama kikubwa  cha siasa Tanzania”alisema Zitto.
    Lakini pia,ameeleza kuwa hakuna kiongozi ambaye ameandaliwa kila chama ana haki ya kugombea nafasi hiyo hivyo basi amewasihi wafanye kampeni kwa uhuru na uwazi.
     Lakini pia,Zitto amewaeleza wanachama kuondoa wasiwasi lakini wahakikishe wanafuata sheria na kanuni za chama kwani kwa yule ambaye atakuwa hajaridhika na matokeo atakuwa na haki ya kupeleka malalamiko katika kamati za Rufaa zilizowekwa kwa kila ngazi.

No comments

Powered by Blogger.