Header Ads

Header ADS

Kassim Majaliwa adai kuta za hospitali ya Wilaya ya Ruangwa zibomolewe.

     Kassim Majaliwa ambae ni Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifanya ukaguzi wa ujenzi wa hospital ya wilaya ya Ruangwa iliyopo mkoani Lindi ameonyesha kutoridhika na baadhi ya majengo hivyo na kutoa agizo kubomolewa.
  Ametoa agizo hilo kwa Tengamaso Wilson ambaye ni Mhandisi wa halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuta zote zenye hitilafu zibomolewe pamoja na kuweka marekebisho katika majengo hayo ikiwemo na kunyoosha kwa kuta.
   Hayo amesema wakati akikagua majengo ya hospitali hiyo, na kumweleza mhandisi kwamba kuta zimepishana unene kwa sababu hakusimamia kazi yake ipasavyo. “Ukuta huu ni mbovu kwa sababu hukuwasimamia vizuri mafundi wako. Kuna mahali juu unaona ukuta ni mdogo na huku chini ni mnene.”

 









    Mara baada ya kuuliza ni kwa nini kumetokea tofauti baina ya kuta hizo, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba tatizo ni upigaji wa lipu. na akatoa agizo “Mhandisi wa Wilaya simamia hili, kagonge upya kuta za jengo hili na lile. Hatuwezi kuwa na jengo la Serikali la aina hii. Tukitoa fedha ya Serikali ni lazima mjiridhishe kama kilichojengwa ndicho sahihi.”
    “Tunahitaji majengo yote yawe ‘smart’, hata ujenzi wake nao uwe ‘smart’. Usikubali kutoa ‘certificate’ kama kazi haijakamilika. Kama kuna kazi haujaridhika nayo, usikubali ‘certificate’ itoke. Zile sentimeta 30 ni lazima zirekebishwe la sivyo, itaonekana huku uliweka matofali mengi kuliko upande ule,” alisisitiza Majaliwa
   Ambapo,Majengo ambayo Waziri Mkuu aliyakagua na kuonesha kutoridhishwa nayo ni ya utawala, wagonjwa wa nje (OPD) na maabara. Majengo mengine yanayojengwa ni jengo la wazazi, la X-ray, la utoaji dawa na la kufulia nguo.
     Akiwa hospitalini hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba katika awamu ya kwanza, Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 na kuelekeza yajengwe majengo saba ya kipaumbele ambayo ni jengo la wazazi, la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, la X-ray, la utoaji dawa, la kufulia nguo na la utawala.
   Ujenzi wa hospitali hiyo unafanyika kwa kutumia njia ya manunuzi inayoitwa ‘Force Account’ ambapo Halmashauri inanunua vifaa vya ujenzi na kuajiri mafundi wa kujenga majengo yaliyoelekezwa wakisimamiwa na wataalamu wa halmashauri na kamati mbalimbali.
    Aidha kwa upande mwingine Waziri Mkuu ametoa agizo kwa Frank Chonya ambae ni mweka hazina katika halimashauri hiyo kuwa kabla hajaamua kutoa fedha za malipo ajiridhishe na kazi za ujenzi zinazofanyika.
       Kwa upande wake  Andrea Chezue ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,sh. bilioni 1.5 alisema ndio kiasi kilichotolewa na Serikali na kimeshatumika lakini pia Halmashauri illitumia zaidi ya sh. milioni 100 ili kusafisha eneo na kulipa fidia ili wapate eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 56.
       Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira.

No comments

Powered by Blogger.