Header Ads

Header ADS

Prof,Joyce Ndalichako ametilia mashaka matumizi ya Fedha Sh.milioni Mia tano

         Joyce Ndalichako ambaye ni Waziri Elimu,Sayansi na Technolojia  ametilia shaka matumizi ya fedha za serikali zaidi ya shilingi milioni mia tano zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa shule ya sekondari Kasangezi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma
         Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya ameagizwa na Ndalichako  kumuondoa mara moja shuleni hapo mkuu wa shule hiyo kwa kushindwa kusimamia vizuri kazi hiyo na pia kuisababishia hasara serikali.















     Akieleza mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi huo Waziri Ndalichako amesema shule hiyo imepatiwa zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4, mabweni 4 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 katika kila moja, matundu ya vyoo 10, bwalo pamoja na ukarabati wa maabara.
       Waziri huyo ameeleza kuwa kazi iliyofanyika haiendani na fedha iliyotolewa kutokana na kujengwa miundombinu hiyo chini ya kiwango
       Milango ya madarasa na hata ya mabweni mmetengeneza kwa mbao laini tofauti na BOQ pamoja na kuwa laini ina uwazi hii nataka itolewe, tazama sakafu imeshaharibika hapa hata mwaka haujaisha mabweni mliniambia ya watu themanini mmejenga ya watu sitini”        
       Kwa mujib wa Ndalichako ameagiza kuwa ujenzi wa mabweni urudiwe kwa kuzingatia BoQ na ameaguza ujenzi huo ufikapo Disemba uwe umekamilika.                                                                                  “Nitakuja mwenyewe mwezi wa kwanza kukagua kama hayo yatakuwa hayajatekelezwa mengine yatafuata,” waziri Ndalichako ameeleza
        

No comments

Powered by Blogger.