Header Ads

Header ADS

Mganga Mkuu Wa Mkoa Wa Songwe Amesema Mila Potofu Ni Chanzo Cha Watoto Kutopata Chanjo

Imesemwa kuwa mila potofu inayoenezwa na baadhi ya wananchi kuwa chanjo husababisha ugumba imekuwa ni moja ya sababu kwa baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto zao kwenye vituo vya afya kupatiwa chanjo za ugonjwa Polio, Sulua na zinginezo.
  Mganga Mkuu Mkoa wa Songwe, Dkt. Khery Kagya alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakidanganywa na watu wanaoendekeza mila potofu kuwa ukimpeleka mtoto kupata chanjo ya magonjwa hayo anapata matatizo ya kiafya ikiwemo ugumba.











Aidha kumekuwepo na Mila nyingine kuwa watoto wa kiume wakipatiwa Tohara uume wao unadumaa na kuwa mdogo hali inayowalazimu baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto wao kupatiwa huduma hiyo ya Tohara.
    Hivyo Kutokana na hali hiyo ya Imani  potofu, wameona ipo haja ya serikali kupitia idara ya afya na wadau wengine kutoa elimu ngazi ya vijiji na kata ili kuelimisha wanannchi hao kuhusu umuhimu wa chanjo  kwa Faida za Afya zao wenyewe.
    “Baada ya kuliona hilo tuanawashirikisha wadau mbalimbali kutoa elimu wakiwemo viongozi wa mila na viongozi wa dini ili kufikisha elimu kwa wananchi hasa sehemu za vijijini” alisema Kagya
   Hata hivyo Alisema wanaendelea pia kutoa elimu kwa uma kupitia wanahabari, mbao za matangazo na vipeperush wakiwa na lengo la kuwafikia watoto wote ambao wanastahili kupata huduma hiyo muhimu.
   "Leo tunazindua chanjo ya Polio, Rubela na Sulua ili kila mtoto kuanzia miezi 9 hadi miaka 5 aweze kupata chanjo kuepuka magonjwa hayo,mwaka 2014 tulichanja kwa asilimia 97,mwaka huu tunatarajia kuchanja asilimia kubwa Zaidi ya hiyo’’alisema Dkt,Kagya.
  Hata hivyo Dkt. Kagya,alisema watoto watakaotibiwa ni 174,115 kati ya hao asilimia 79 walizaliwa kwenye vituo vya kutolea tiba na asilimia 21 walizaliwa kwa wakunga wa jadi ambapo wao wanapata taarifa kupitia kwa watoa huduma za jamii ngazi ya vijiji.
  Dkt.Kagya Aliongeza kuwa  toka mwaka 1996 Tanzania haijawahi kuwa na watoto wenye magonjwa hayo na kwamba,wamekuwa wakitoa chanjo na kufanya ufuatiliaji ili kubaini watoto waliokumbwa na ugonjwa huo lakini hawajawahi kukuta na wao wanaendelea kutoa chanjo ili magonjwa hao yasitokee.
   Aidha Akizungumzia hali ya mikakati ya serikali kupitia idara ya Afya,Dkt,Moses Lyimo,Mr atibu wa huduma za chanjo mkoani Songwe,alisema wamejipanga kuwapatia chanjo hizo watoto wote kwenye vituo vya kutolea tiba na wale ambao maeneo yao hakuna vituo hivyo watawafikia kupitia huduma tembezi.
   Alisema Chanjo ya Sulua Rubela,inamhusu mtoto kuanzia miezi 9 hadi miaka 5 na Chanjo ya Polio mtoto kuanzia miezi 18 hadi 42 na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanaandikisha watoto kwa asilimia Zaidi ya 100 ukilinganisha na mwaka 2014 walipoandikisha kwa asilimia 97.
   Daniel Mwashiuya, Mkazi wa Mbozi, akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake,alisema anaipongeza serikali kupitia idara ya afya kwa kuona umuhimu wa uhai wa watoto wao,na kusema kuwa kutokana na chanjo hizo,magonjwa hayo yametoweka 

No comments

Powered by Blogger.