Header Ads

Header ADS

Kassim Majaliwa atembelea Bandari ya Mtwara.

    Kassim Majaliwa,Waziri Mkuu amewasili katika Bandari ya Mtwara ambapo ameweza kuona shehena ya korosho zilizonunuliwa na kampuni la Tang Long zikisafirishwa kupeleka Nchini Vietnam kwa kutumia usafiri wa Meli kubwa inayojulikana kwa jina la As Christiana.
      “Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu. Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu''.














Aidha,lengo kubwa la Waziri mkuu kutembelea katika Bandari hiyo ni kuangalia kazi za usafirishaji wa korosho unavofanyika hata hivo amesema kuwa amefurahishwa na kuridhishwa  na kasi pamoja na utaratibu unaoendelea Bandarini hapo hadi sasa.
     Hata hivyo,amesema kampuni ya Tang Long ya nchini Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini na kwamba wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.
  Lakini pia,Kassim majaliwa ameeleza suala la kuongeza thamani katika ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini,na kuandika kwenye vifungashio ili dunia nzima kiujumla itaweza kutambua kuwa korosho hiyo inatoka Tanzania pia kwa namna hiyo ilaongeza kukuza soko.
   Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje
      “Wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda  unalenga katika kuongeza  ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji.”Amesema Waziri mkuu
  Lakini kwa upande wake Geoffrey Mwambe amaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekrzaji Tanzania ameeleza kuwa licha ya Kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini pia imeomba Serikali ikodishiwe Kiwanda kimojapo Kampuni hiyo  ili waweze kuanza ubanguaji wa korosho ikiwa ni mpango wa muda mfupi na katika mpango wao wa muda mrefu wameomba wajenge kiwanda cha kubangulia korosho katika maeneo ya Mkoa wa Mtwara au Lindi .

No comments

Powered by Blogger.