Header Ads

Header ADS

Afisa Tarafa atoa Onyo kwa Watumishi wanaonyanyasa wazee

Titho Cholobi ambaye ni Afisa Tarafa wa Elerai,amewaonya baadhi ya Watumishi hususan watumishi wa afya wanaowawalazimisha wazee kuchangia katika huduma za afya ili watibiwe kinyume na taratibu ambapo wazee wanatakiwa watibiwe bila malipo yoyote.












Ameyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha siku ya wazee katika shule ya Parent Afisa Titho ameeleza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wale wote wanaokiuka sheria na maelezo ya Serikali kwani wazee wana mchango mkubwa sana katika taifa.
  Pia ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakumba wazee ili kuwepo na haki na usawa.hata hivyo wazee wa kata ya sokoni one jijini Arusha wamesema kuwa wanaiomba Serikali kushughulika na watumishi wa vituo mbalimbali vya afya ambao wamekuwa wakiwataka wao kuchangia gharama za matibabu.
  Baadhi ya wazee ambao ni Tabu Said na Gerald Machafuko ni baadhi ya wazee ambao wameshiriki katika hafla hiyo na wamesema kuwa suala kupatiwa matibabu limekuwa ni changamoto inayowakumba wazee wengi jambo ambalo linawapelekea wao kushindwa kwenda katika vituo vya afya kupata matibabu kwa kuhofia kulipa gharama.
“Jicho langu lina matatizo mikono yangu ilikufa gansi yote miwili nilipoenda hospitali dirishani niliambiwa nilipe shilingi elfu thelasini mimi hiyo hela naitoa wapi na mmenipiga picha na kitambulisho mkanipa”Alisema mzee Tabu said kwa machungu.
   Aidha mwenyekiti wa Baraza la wazee katika kata ya sokoni one Paul Moshi ameiomba Serikali kuwajengea Zahanati mpya ili kuwarahisishia wao kupata huduma kirahisi.
   Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa huyo amesema kuwa kwa sasa wameanza utaratibu mpya wa kuwapa vitambulisho na hawajawahi kupata malalamiko ya wazee ambao wametozwa fedha pindi wanapoenda kupata matibabu.
    Imetolewa na Mwandishi Diana Malekela.

No comments

Powered by Blogger.