Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaweka saini katika ujenzi wa mji wa Kwahani.
Iddy Haji Makame ambaye ni Naibu katibu Mkuu katika Wizara ya fedha na mipango Zanzibar ameambia wananchi kuto kuwa na wasiwasi kutokana na kuvunjiwa kwa nyumba zao kwani Serikali ina malengo makubwa hususani kuwajengea nyumba za kisasa pia zilizo bora.
Hayo amezungumza wakati akiwa katika mji wa mpya wa nyumba za kisasa ambao unajengwa Kwahani wakati wakitiliana saini na Kampuni ya Estim Constraction LTD ya Dar es salaam ambayo inashughulika na Ujenzi huo.
Lakini pia,amesema kuanza kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya nyumba tano za ghorofa nne kila moja na maduka eneo eneo la chini ni uamuzi wa Serekali wa kuwawekea mazingira mapya kisasa na kuwaondeshea mazingira yale ya zamani.
Aidha,amewaeleza wananchi wa mji huo kwamba kampuni hiyo wamekubaliana kuwa watakamilisha ujenzi huo kwa muda wa mwaka mmoja lakini pia Kampuni hiyo ina udhoefu mkubwa sana.
Pia,amesema waweke matumaini ya kuishi katika mazingira bora na ya kisasa huku wakiendelea kuvuta subira.
Razalo Peter ambaye ni msimamizi wa ujenzi huo amewaeleza wananchi wa Kwahani kwamba ili kazi iweze kwenda hara hatimaye kukamilika kwa muda uliopangwa wananchi wa eneo hilo wanatakiwa kutoa ushirikiano hususani katika kipindi hiki cha ujenzi.
Aliwapa matumaini makubwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwamba watapata nyumba bora na za kisasa katika kipindi cha muda mfupi ujao.

Sheha wa Shehia ya Kwahani Machano Mwadini Omar ameishauri Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo kuwatumia vijana wa eneo hilo katika kazi zisizohitaji utaalamu ili nao kutokana na mradi huo waweze kunufaika.
Lakini hata hivo amesema kuwa nyumba zilizovunjwa kwa ajili ya kupisha ujenzi mpya zilikuwa na vijana wengi waliokuwa wakiendesha shughuli zao za maisha na hivi sasa hawana kazi maalum hivyo iwapo watapatiwa kazi wakati wa ujenzi zitawasaidia kimaisha.
Ali Hamad Haji na Hija Sudi Juma hao ni baadhi ya wananchi waliovunjiwa nyumba zao lakini wameeleza kwamba kuvunjiwa kwa nyumba zao kwa kiasi kidogo imeleta shita lakini wameiomba Serikali mara ujenzi utakapokamiliza ifanye uadilifu huku wao wataendelea kuvuta subira.
Vilevile wametoa pongezi kwa Serikali kwa kupatiwa pesa ili waweze kutafuta makazi ya muda huku wakiendelea kusubiri makazi mapya.
Katika utaratibu wa utiaji wa saini kampuni ya Estim Constraction LTD ikiwakilishwa na meneja mkuu wa kampuni hiyo ambaye ni Girdhar Pindolia huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Iddy Haji Makame ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha.
Imeandikwa na mwandishi;Adolf Mwingira.
No comments
Post a Comment