Header Ads

Header ADS

Kitambulisho Cha NIDA Na Cha Kupigia Kura Kutotumika Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa.

   Serikali Mkoani Pwani, imetoa rai kwa wananchi kupuuza baadhi ya watu wanaowahadaa kuwa kitambulisho cha Taifa -NIDA na cha kupiga kura wataweza kupigia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji Novemba 24 mwaka huu,suala ambalo ni baadhi ya watu wamelipotosha.


 










Aidha imeweka wazi kuwa takriban watu 680,000 wanatarajiwa kujiandikisha kwenye daftari hilo, hivyo wamehamasishwa kujiandikisha ili kuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.
   Pia akizidi kuhamasisha umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo hadi octoba 14 mwaka huu ,wakati alipokwenda kutimiza haki yake ya msingi kujiandikisha kituo cha Mwanalugali ‘A ‘ Kibaha ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema kitambulisho cha Taifa na cha kupigia kura havitahusika katika Zoezi la kupiga kura.
   “Nimetumia haki yangu ya msingi kujiandikisha ,nimejiandikisha wa 123  lengo la kituo hiki ni kuandikisha watu 1,332 na kimkoa tunatarajia kuwa na watu 680,000 ,alifafanua Ndikilo.
  “Wapo baadhi ya watu wanahadaa wenzao kwamba hakuna ulazima wa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi na badala yake watatumia vitambulisho kama si cha uraia basi cha kupiga kura,sio kweli mtapoteza haki yenu ya msingi.”
  Lakini  Hata hivyo Ndikilo alieleza ,suala la kupiga kura ni la wananchi wote siyo la watu wachache ili kuondoa malalamiko kuwa viongozi waliochaguliwa hawafai wakati wao hawakushiriki hilo ni tatizo.
  Alieleza Pia  taratibu zote zimekamilika ikiwa ni pamoja na fedha ambapo wasimamizi tayari wameshateuliwa  kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.  

No comments

Powered by Blogger.