Header Ads

Header ADS

Serikali yatoa wito kwa wananchi na watumishi kujiandikisha kwenye daftari ya wapiga kura.

    Ramadhani Kailima ambae ni Waziri wa mambo ya ndani ya nchi amewataka watumishi wa umma pamoja na wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kuweza kutumia fursa hii kuchagua viongozi wenye sifa katika Serikali za mitaa.
   Amezungumza hayo wakati akiwa mjini Dodoma baada ya kujiandikisha katika daftari hilo kwenye kituo kilichopo Mtaa wa Chimuli, kata ya Makole.
  Ambapo amesema uchaguzi huo wa Serikali za mitaa una mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu, lakini uzoefu unaonyesha kuwa kuna mwamko mdogo kwa kundi la watumishi wa umma kujiandikisha, kushiriki uchaguzi huo ili waweze kuchagua viongozi wenye sifa.












  “Kampeni zitafanyika kwa wiki moja kuanzia Novemba 17-23, mwaka huu, uchaguzi utafanyika Novemba 24, mwaka huu…ni muhimu jamii kutambua kuwa, mshindi katika uchaguzi huu atapatikana kwa idadi ya wapiga kura sio asilimia,” amesema Kailima.
    Aidha,Kailima amesema ni muhimu Watanzania wakashiriki uchaguzi huo uli watumie fursa hiyo kuchagua kiongozi anayestahili, wasiposhiriki atachaguliwa Mwenyekiti wa Serikali ama mjumbe ambaye jamii kubwa haitapenda achaguliwa.
    “Nawaomba wananchi wahudhurie kampeni, waulize maswali kwa wagombea, watumie fursa hiyo kuchagua viongozi ambao ni waadilifu na waaminifu.”
    Lakini pia, Kailima amewaonya wananchi kutojihusisha kupokea rushwa kutoka kwa yeyote. “Rushwa ni adui wa maendeleo, wananchi mjiepushe kupokea rushwa, Wizara yangu kupitia taasisi zake za ulinzi na usalama ziko imara, tutaimarisha ulinzi wakati wa kampeni, upigaji kura na utangazaji matokeo,” alifafanua
   Vilevile Kailima ametoa pongezi kwa wasimamizi wa zoezi hili pamoja na waandikishaji kwa kuudhurulia mapema katika vituo vyao vya uandikishaji.
  Aidha,Kailima ameeleza kwamba  uandikishaji huo hauna vikwazo kwani hauhitaji kitambulisho cha uraia, cheti cha kuzaliwa kwani vituo vya uandikishaji vipo barabarani lakini pia mitaani.
   Imeripotiwa na Mwandishi wako Adolf Mwingira.

No comments

Powered by Blogger.