Maduka Dar es Salaam Kufunguliwa Saa 5 Kesho.
Mhe,Paul Makonda amesema kuwa siku ya kesho maduka yote ya mkoni humo yafunguliwe saa 5 asubuhi ili kupisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuenzi miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa.
Ametoa agizo hilo leo Jumapili Oktoba 13,2019 kupitia Taarifa yake katika vyombo vya habari.
Aidha, Makonda ameeleza kuwa ikiwa kesho ni siku ya kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni vizuri wananchi wote wakamuenzi Baba wa Taifa kwakuhakiksha muda wakutosha kwa kujiandikisha kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ili waweze kuchagua viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Hata hivyo,Makonda amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, Shule za Msingi, sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya kujiandikisha.

No comments
Post a Comment