Header Ads

Header ADS

Seleman Jaffo ametaja mikoa ambayo haifanyi vizuri katika zoezi la uandikishaji.

     Seleman Jafo ambaye ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa ametoa orodha ya mikoa ambayo haifanyi vizuri katika jukumu la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajiri ya kufanya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
  Aidha ameeleza kwamba amuomba Rais Magufuli kuchukua hatua kali kwa viongozi mikoa na wilaya ambazo zitashindwa kuandikisha kwa asilimia 50.
   Akitoa taarifa ya maendeleo ya uandikishaji wa wapigakura, Jafo amesema tangu kuanza kwa uandikishaji Oktoba 8 hadi 14 mwaka huu baadhi ya mikoa imefanya vibaya.
  Hata hivyo,Jaffo ameeleza mikoa mitatu ambayo amefanya vibaya ambayo ni  Dar es salaam, unaoongozwa na Paul Makonda, ambao umefanikisha kwa asilimia 8, Kilimanjaro unaioongozwa na Anna Mghwira kwa asilimia 12, na Arusha unaoongozwa na Mrisho Gambo kwa asilimia 13.
  Jaffo amesisitiza kuwa atampelekea Rais Magufuli dokezo kwa mikoa itakayoshindwa kufanya vizuri katika uandikishaji wapigakura katika uchaguzi huo ili achukue hatua.
  Aidha Jafo amesema, wapo wakuu wa mikoa wanaoweza kuhamasisha watu kujaa uwanjani siku ya mechi za mpira ila suala la kujiandikisha wapigakura wanasuasua.
    Ametaja mikoa ambayo imefanya vizuri kwa kujiandikisha zaidi ya asilimia 53 ni Iringa, Songwe, Mbeya na Tanga, na hadi sasa jumla ya watu milioni 5.8 wamejiandikisha.
      Lakini pia wananchi ambao wanatarajia kufanya uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24,mwaka huu ni zaidi ya watu milioni 20 wanaotarajia kushiriki uchaguzi huo.

No comments

Powered by Blogger.