Header Ads

Header ADS

Magufuli ameagiza Kamanda wa Polisi atumbuliwe Sumbawanga.

   Rais Magufuli ameagiza kamanda wa polisi wa Wilaya ya Sumbawanga, Polycarp Urio kusimamishwa kazi  kwa madai ya kushindwa kutekeleza maagizo aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.
      Kwa mjibu wa taarifa agizo la Urio aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa kusimamishwa kazi limetolewa leo Jumapili Oktoba 4, 2019 baada ya Rais Magufuli kumpigia simu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na kumtaka kumsimamisha kazi Urio.
  
   Pia itakumbukwa kuwa Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.

Leo akiwa kwenye uzinduzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga,  Rais Magufuli alimuuliza kamanda wa polisi wa mkoa huo,  Mathias Nyange kuhusu askari tisa hao ila alionyesha kutofahamu chochote.

“Sina majina yao, na bahati mbaya sifahamu chochote sikuwepo ofisini aliyekuwepo hakunipa taarifa yoyote kuhusu maelekezo hayo,” amesema Kyando. Baada ya majibu hayo Rais Magufuli alimpigia simu IGP Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi Urio.

Rais Magufuli alimuagiza RPC wa Rukwa, Mathias Nyanda kutekeleza agizo la Waziri Lugola la kuwahamisha vituo vya kazi askari hao 9 wanaotuhumiwa kuwabambikiza kesi wananchi

No comments

Powered by Blogger.