Header Ads

Header ADS

Watumishi 48 Iramba wanatakiwa wachunguzwe na Takukuru Kwa upotevu wa Fedha.

    Kassim Majaliwa ametoa agizo mkoani singida kwa Kamanda wa TAKUKURU Bw.Adili Elinipenda achunguze Watumia 48 ambao wnasadikika kuhusika na udanganyifu katika kupotea kwa Fedha.
    Wakati akizungumza na madiwani pamoja na watumishi leo hii katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmshauri hiyo ambapo agizo hilo ametoa.
  Aidha,Majaliwa ameeleza sehemu saba ambazo zinatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini upotevu huo wa fedha.Ambapo amesema Eneo la kwanza ni upotevu wa makusanyo ya ndani kupitia mawakala wa ukusanyaji mapato (POS) ambapo mawakala wanaokusanya fedha wanashirikiana na watumishi wa Halmashauri na kuzitumia bila kuziingiza benki.











   Katika kundi la watumishi 10 wakiongozwa na mtu wa TEHAMA, wameshirikiana kupata password na fedha zikishakusanywa wanazitoa na kuzitumia bila kuzipelekea benki. Wamesahau kwamba malipo yalipoingizwa mara ya kwanza, data ilirekodiwa kwenye mfumo wa malipo na sisi tunaona ni kiasi gani kimekusanywa.”
     Aidha,watumishi hao ambao ni Adam Mzengi(Mhasibu kahamishiwa Gairo); Rafaeli Nasari; Caroline Makundi (kahamishiwa Singida Manispaa), Edson S. Ally (Afisa Biashara);Salum Omari (Mtaalamu wa TEHAMA); Martin Kimisho (Mhasibu Msaidizi); Prosper Banzi (Afisa Biashara); Hassan Ponda (Mhasibu kituo cha afya Ndago); Hafidh Ngayunda (Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya) na Muhidin Mohammed (Mweka Hazina wa Wilaya) ambaye tayari amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma hizo.
    Ambapo Waziri mkuu  ameagiza Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya akae pembeni hadi uchunguzi wa TAKUKURU utakapokamilika kutokana na upotevu wa fedha hizo.
   Lakini pia,Waziri Mkuu amebaini mchezo mwingine uliochezwa na watumishi wa halimashauri hiyo,ambapo ameeleza kwamba kuna watumishi 38 ambao walilipwa kiasi cha sh milioni 46 ambazo zilikuwa sehemu ya sh. milioni 400 za kujenga vituo vya afya vya Ndago na Kinampanda wilayani humo.
   “Hapa nina vocha zote za malipo walipeana fedha watu hawa akiwemo Mkurugenzi wao. Lakini ni kazi gani ambayo kundi lote hili lilikuwa likiisimamia na kustahili kupata malipo hayo? Kutoka makao makuu ya wilaya hadi Ndago au Kinampanda kuna umbali gani?” alihoji Waziri Mkuu.
      “Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi, fuatilia wote waliohusika sababu majina tunayo, kama hawastahili kulipwa ni lazima warudishe fedha yetu. Hii ni sehemu ya sh. milioni 90 ambazo hazijulikani ziliko na zilikuja kujenga kituo cha afya. Fedha hizi zimekuja na maelekezo rasmi, ni kwa nini zilibadilishwa matumizi,” alisema Waziri Mkuu.
   Hata hivyo,Majaliwa amsema kulikuwa na shilingi milioni 29 ambayo ilitumwa na TAMISEMI kwa ajili ya kulipa likizo za walimu lakini Mkurugenzi alitumia kulipia usafirishaji wa makontena ya vifaa vya tiba kutoka Sweden hadi Singida wakati mkataba wa malipo unasema Halmashauri ilipaswa kulipia kutoka bandari ya Tanga hadi Singida.
     “Hii fedha ya walimu ya likizo nataka irudishwe mara moja. Pia kuna shilingi milioni 6.86 ambazo mmedai ni malipo ya kukomboa mizigo bandarini wakati vifaa hivyo vilipata msamaha wa kodi. Tena kuna sh. milioni 34 ambazo zililetwa kurekebisha Ikama za walimu lakini hadi leo hazijalipwa. “Kamanda wa TAKUKURU nataka uniambie nafasi ya Afisa Elimu ikoje kwenye suala hili,” Waziri Mkuu alieleza.
   Lakini pia,alizungumzia fedha iliyoletwa kwa ajili ya ujenzi wa machinjioni ambayo hadi sasa haijakamilika “Hivi mnachangisha watu sh. 30,000 kwa ajili ya kupata dawa wakienda kutibiwa lakini leo hawana dawa kwa sababu mmezitumia ndivyo sivyo na wao hawana dawa kwenye vituo hivyo kwa sababu hamjazirejesha.”
   “Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi kwenye fedha ya mikopo ya akinamama, vijana na wenye ulemavu ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri. Fedha hii haijatoka tangu mwaka 2017/2018 na 2018/2019.''Alisema Majaliwa
     Imelipotiwa na ripota;Adolf Mwingira
       

No comments

Powered by Blogger.