Header Ads

Header ADS

CHADEMA wapata pigo tena Mwenyekiti atimkia CCM.

   Edwirn Enosy Swale (Wakili)aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA wa pili katika Mkoa wa Njombe ambapo aliyeshika nafasi baada ya Fakih Lulandala kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM naye pia leo hii amejiuzulu chama hicho na Kuunga mkono chama cha Mapinduzi CCM.
   Baada ya kupokelewa,kuapishwa na kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi katika Ofisi za CCM Wilayani Njombe ambapo amezungumza akisema baada ya kuona jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuleta maendeleo nchi naye ameamua kuunga mkono juhudi hizo.















   “Mimi kama kijana nimeamua kwa dhati kutumikia nchi yangu katika chama ambacho kwa sasa kimekuwa na muelekeo wa kusaidia wananchi,na nitoe wito kwa vijana wote nchini na watanzania kwa ujumla wake,tusije tukapoteza fursa ya kutokumtumia Magufuli kuipeleka nchi yetu katika hali neema”alisema Swale
   Lakini pia,Chama cha mapinduzi kimempokea Msafiri Peter Mpolo aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) jimbo la Lupembe ambaye amesema ameamua kuhama chama hicho kutokana na kuto kuwepo kwa ajenda za kusimamia kwa sasa.
   “Tumeona hakuna sababu ya kuendelea chama cha upinzani kutokana na mambo makubwa ambayo yamefanywa na serikali kwa sasa,ukienda Makete utaona barabara zinavyojengwa,watumishi wamekuwa na nidhamu kubwa,hizo ndio ajenda tulizokuwa tunasimamia lakini leo hii nikibaki Chadema nitasimamia nini”alisema Msafiri Peter Mpolo
     Aidha,Edward Mgaya ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Njombe mara baada ya kuwaapisha na kuwakabidhi kadi wanachama hao,amemtaka Swale kuunganisha nguvu zake pamoja na kushirikiana na Jorum Hongoli, ambaye ni Mbunge wa jimbo Lupembe katika kuweza kuleta maendeleo zaikwenye jimbo hilo la Lupembe.

No comments

Powered by Blogger.