Header Ads

Header ADS

Makamu Wa Rais Autaka Umoja Wa Wanawake Tanzania(UWT) Kuwa Mstari Wa Mbele Kuwakomboa Wanawake Kisiasa

  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alifungua mkutano wa siku mbili wa wabunge wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA), na kuutaka Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuwa mstari wa mbele, kuwakomboa wanawake kisiasa ili washiriki katika chaguzi mbalimbali.


 Aidha,Mkutano huo unawashirikisha wabunge wanawake kutoka mataifa yaliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara.Makamu wa Rais aliwataka wanawake, kushirikiana katika kusimamia demokrasia katika mataifa hayo ya Afrika, kwani wanakabiliwa na changamoto nyingi wanapoamua kujihusisha na masuala ya siasa katika nchi zao.

Pia,Alitaja baadhi ya changamoto zinazowapata ni vitendo vya kunyanyaswa pale wanapoamua kugombea nafasi yoyote wakati wa mchakato wa uchaguzi.

"Viongozi wanawake ni watu muhimu katika Taifa lolote barani Afrika katika kusimamia amani, utulivu na mshikamano katika jamii," alisisitiza Makamu wa Rais.

"Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani mwaka 2015 chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli imepanua wigo wa kuwepo na idadi kubwa ya viongozi wanawake katika nafasi ya uongozi, nafasi za utoaji wa maamuzi, madiwani na wabunge," aliongeza.

Hata hivyo,Alisisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria kwa dhati kupanua wigo wa kuongeza nafasi za viongozi wanawake wakiwamo wabunge kwa lengo la kuweka usawa kati ya wanaume na wanawake katika uongozi.

Aidha, alisema Tanzania imedhamiria kuongeza nafasi za wabunge wanawake ambao kwa sasa idadi ya wabunge wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ni 145 sawa na asilimia 36.9 kati ya wabunge wote 393.

 Samia Alisema kutokana na hali hiyo, Tanzania ni nchi ya tano katika nchi za Jumuiya ya Madola barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya wabunge wanawake.

Hata hivyo, Makamu wa Rais alisema kumekuwapo na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na kuwekewa vikwazo vingi pale wanawake wanapojitokeza kugombea nafasi wakati wa michakato ya chaguzi.

 Lakini,Alitoa wito kwa UWT kuhamasisha watoto wa kike kuanzia ngazi za chini ili washiriki kikamilifu katika nafasi za kisiasa na uongozi kuanzia ngazi wanapokuwa shuleni ili kupata uzoefu Zaidi.

No comments

Powered by Blogger.