Header Ads

Header ADS

Mashujaa FC Yapokea Kichapo Dhidi Ya Simba SC

 Sharaf Shiboub ameipa Ushindi Simba SC Kwa Bao La Kipekee mnamo dakika ya 56 kipindi cha pili, Bao Hilo limeipa ushindi timu hiyo dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa kirafiki  uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Hii Leo.














Hata hivyo Simba imecheza mechi yake ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara msimu huu.
   Katika mchezo huo, uwanja wa Lake Tanganyika ulionekana kuwa na changamoto haswa kwa Simba kutokana na vipara vingi na sehemu kadhaa zikiwa hazina nyasi.
   Aidha Mapema baada ya mechi kumalizika, Beki Yusuph Mlipili, amesema wangeweza kushinda zaidi ya bao tatu lakini uwanja ulikuwa shida kwao jambo lililopelekea wao kutopata Bao la tatu.
  "Uwanja kwakweli upande wetu ulikuwa na changamoto nyingi.
  "Tungeweza kushinda zaidi ya bao tatu, hii imepelekea tushindwe kucheza kama ambavyo tumezeoa kucheza siku zote," amesema Mlipili.

No comments

Powered by Blogger.