Header Ads

Header ADS

Mafuriko yaua watoto watano Tanga.

  Mafuriko Wilayani Korogwe Mkoani Tanga yaua watoto watano mkoani humo na kusababisha idadi  ya waliofariki kwa mafuriko kufikia watu 12 hadi sasa.
  Vifo hivyo vimetokea katika kata ya Foroforo,ikiwa ni baada ya nyumba moja iliyokuwa na wanafamilia 8 kuanguka nakusomba watoto wa 5  ambapo miili yao  imepatikana










Kulingana na mvua hizo zinazo endelea kunyesha mkoani humo  takribani wiki mbili sasa katika maeneo mbali mbali,  kaya zaidi ya 300 zimekosa makazi mkoani humo.
      Hata hivyo daraja la Mto Mandera lililopo kata ya Segera mpakani mwa wilaya ya Handeni na Korogwe limekata mawasiliano jana, ya barabara kati ya mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Arusha, Pwani na Manyara na kusababisha magari zaidi ya 200 kukwama kwa zaidi ya saa 36 huku abiria zaidi ya 800 wakilala nje.
   Aidha, watu 120 ambao makazi yao yamezingirwa na maji wamehifadhiwa katika kambi maalumu, kijijini hapo na kutakiwa kutorudi katika makazi yao hadi tamko la Serikali litakapotolewa Ndipo watakaporuhusiwa kurudi makwao.

No comments

Powered by Blogger.