Header Ads

Header ADS

Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi Ya Maji Watakiwa Kuongeza Kasi

   Wakandarasi wanaotekeleza Miradi Ya Maji Kwenye Wilaya Za Newala,Tandahimba na Masasi Mkoani Mtwara wanatakiwa kuongeza kasi ya ytekelezaji wake ili kukamilisha Miradi hiyo mapema iwezekanavyo.


















     Agizo hilo limetolewa na Mhandisi Anthony Sanga ambaye ni Naibu Katibu Wizara Ya Maji Mkoani Mtwara kwa nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye miradi ya maji inayotekelezwa kwenye wilaya hizo Hivi Karibuni.
    Sanga alitembelea mradi wa Mkwiti uliyopo Wilaya ya Tandahimba, Chanzo cha Maji cha Mitema, Mradi wa Makonde na aMradi wa Kilidu yote ya Wilaya ya Newala na mradi wa Chipingo Wilayani Masasi Akikagua Utendaji Wa Kazi.
     Hata hivyo Mara baada ya kuzungukia miradi, Mhandisi Sanga alisema hajaridhika na kasi ya utekelezaji wake licha ya kwamba vifaa vinavyohitajika kukamilisha miradi hiyo ikiwemo mabomba na mitambo ya kusukuma maji vikiwa vimekamilika.
      Aliongeza kuwa haoni sababu kwanini miradi inatekelezwa kwa kusuasua licha ya kuwa vifaa muhimu vipo eneo la mradi. "Nimezungukia maeneo ya miradi nimeona vifaa muhimu vinavyohitajika kukamilisha miradi vipo, hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda," alisisitiza Mhandisi Sanga.
  Alisema kinachotakiwa ni Wananchi kupata Maji mapema Na suala la kutotekeleza  Mradi huo kwa Haraka halitokubalika kabisa hivyo wakandarasi wanatakiwa kufanya haraka iwezekanavyo kukamilisha Miradi hiyo ili kuepukana na changamoto za maji.
   Aliagiza wasimamizi wa miradi ambayo ipo katika hatua ya ulazaji bomba kuharakisha kumaliza shughuli hiyo hasa ikizingatiwa msimu wa mvua umefika na kwamba mitaro hiyo ikiendelea kubaki wazi itajifukia na italazimika kuchimbwa upya.
  "Nimeona mitaro imechimbwa na imekamilika na mabomba yapo hakikisheni kuanzia sasa mabomba yanalazwa ili kuepusha gharama ya kufanya kazi mara mbili ya kuchimba mitaro ya maji," aliagiza Naibu Katibu Mkuu Sanga.
    Aidha  Mhandisi Sanga aliagiza wasimamizi wa miradi kuhakikisha kwenye kutekeleza miradi wanaanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili wananchi waanze kupata huduma na baadaye waendelee na maeneo mengine wakati ambao tayari wananchi wanakuwa na huduma.
  “Mnatakiwa kuwa wabunifu wakati wa ujenzi wa miradi, mnapaswa kuanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili kwanza wananchi wapate huduma na huku mkiendelea kutekeleza maeneo mengine,” alisisitiza Mhandisi Sanga.
    Mhandisi Sanga yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa Mkoani humo ili kujionea hatua ya utekelezaji wake sambamba na kufahamu changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi mapema.


   













 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye kituo cha Mtongwele ambacho kitatumiwa kupelekea maji kwenye mradi wa Mkwiti kutokea chanzo cha Mitema (Mitema Well Field). Kulia ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

 











  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akikagua mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata wa Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara unaotumia maji kutoka Mto Ruvuma.

No comments

Powered by Blogger.