Header Ads

Header ADS

Mila Makovec Mwenye Ugonjwa Wa Ubongo Apewa Dawa Ya Kipekee

Mila Makovek ambaye ni Msichana Wa Miaka Nane Amekuwa akisumbuliwa na Ugonjwa hatari ambao umekuwa hautibiki.
   Madaktari wa watoto katika hospitali ya Boston waliamua kutengeneza dawa inayoweza kutumika kwenye vina saba vya mtoto huyo peke yake kwa ajili ya kuokoa maisha yake.Lakini hivi sasa Mtoto huyo anaendelea Vizuri.











 Hata hivyo Ugonjwa huu ni nadra sana kwa mtu kuupata na huwa unamfanya mtu kuwa na wasiwasi au mshtuko na mara nyingi hupelekea mtu kufa.
   Ugonjwa anaosumbuliwa na mtoto huyo huwa unatokea kwa watu wachache sana katika umri wa kati ya miaka 5-10. Kuna aina nyingi za ugonjwa huu na mtu anaweza kupona mpaka anapofika miaka 20.
  Ugonjwa huu hatari huathiri ubongo na mfumo wa seli za neva na hata macho.
    Msichana huyo alianza kuugua akiwa na miaka mitatu kipindi ambacho mguu wake wa kulia ulipoanza kupinda.
    Mwaka mmoja baadae, alihitajika kusogeza kitabu kwa karibu kabisa na macho kwa sababu alianza kuwa na uhafifu wa kusoma na alianza kutembea kiajabu.
   Alipofika miaka sita, Mila alikuwa kipofu na aliongea kwa tabu sana na alikuwa anashtuka mara kwa mara.
   Familia Ya Mila Waliamini Kuwa Huo ni Ugonjwa Unaoathiri Maumbile hivyo wakaanza Kampeni iitwayo Mila's Miracle Foundation kwa matumaini kuwa mtoto wao atapona na kurejea katika hali yake.
   "Nilikuwa katika mlo wa jioni, mimi na mke wangu akanionesha picha ambayo ilikuwa imewekwa na rafiki yake kwenye Facebook kuwa familia hiyo ilikuwa inatafuta msaada," Dkt. Timothy Yu aliiambia BBC.
  Daktari huyo alikutana na Mila kwa mara ya kwanza mwezi Januari mwaka 2017.Timu ya madaktari huko Boston walifanya uchunguzi wa vina saba vya Mila na kubaini sehemu ya kipekee katika mwili inayosababisha ugonjwa huo.Baada ya kuona matokeo ya utafiti huo , wanasayansi waliona kuwa inawezekana kumtibu.
   Hivyo wakaamua kubuni dawa ambayo waliijaribu kwa Mila na kwa wanyama wa Maabara na ithibitisha kwa ajili ya matumizi na mamlaka ya  Chakula na dawa Nchini Marekani.
    Mila alianza kutibiwa na dawa inayoitwa Milasen tarehe 31 Januari mwaka 2018.
   Kwa kawaida dawa huwa inachukua muongo au nusu ya muongo kutoka maabara na kuanza kufanyiwa majaribio kwa wagonjwa.
   Lakini timu ya wanasayansi hao wa Marekani wameweza kufanikiwa ndani ya mwaka mmoja tu.
    "Tulipomaliza na kuangalia nyuma, tulishangazwa sana na kujivunia kazi tulioifanya. Mara nyingine ni vyema kuwa mwerevu zaidi kwa sababu maisha ya mtoto yalikuwa hatarini na tulikuwa tunafanya kazi kwa bidii ili kila mtu afanye kazi katika upande wake kwa haraka," Dkt Yu alisema.
   "Hatuna uhakika kama kuna dawa aina hii iliwahi kubuniwa kabla", aliongeza Dkt Huyo
Aidha dawa hii haiwezi kumsaidia Mila athari zote alizonazo,"Kwa Mwaka Wa Kwanza Tulianza Kuona maendeleo Kidogo Ugonjwa huu kupona kabisa kwake sio rahisi" Dkt aliiambia BBC.
   Pia Familia Yake iliripoti kuwa Mila ameanza kupata nafuu kwa kusimama vizuri na kumeza chakula.
   Kuna dalili kuwa katika mwaka wake wa pili wa matibabu kutakuwa na maendeleo makubwa zaidi kama Mila ataendelea kuangaliwa kwa ukaribu.
  "Tunadhani kuwa tiba yake inaenda polepole na tuna matumaini kuwa inaweza kumpa nafuu," Dkt. Yu alisema.
  Hata hivyo daktari anaamini kuwa kama ugonjwa kama huu utatokea kwa mtu mwingine, itakuwa rahisi kupatiwa tiba mapema na kuweza kuweka utofauti mkubwa.
   Aidha watafiti hawawezi kutaja gharama walizotumia kutengenezea dawa hizo.
     "Tusingeweza kuchukua hatua ya kuitengeneza kama tusingeona njia nzuri ya kuifanya dawa hii ipatikane kwa urahisi.Wazo la dola milioni kwa ajili ya mamilionea halipo kwa kile tunachokifanya", Dkt. Yu alisema.

No comments

Powered by Blogger.