Header Ads

Header ADS

Mkutano wa Mbunge wa Iringa Mjini wazuiliwa na Jeshi la Polisi.

   Mkutano wa mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA)Mchungaji Peter Msigwa umezuiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa wakidai kwamba kutowepo kwa Askari wa kutosha kwa ajili ya ulinzi katika mkutano huo.
   Ambapo taarifa hizo za kuzuia kwa mkutano huo zimesamba katika mitandao ya kijamii ikionyesha barua ya zuio kutoka Polisi katika viwanja vya Mwembetogwa ndipo mkutano huo ulitakiwa ufanyike.
   Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Juma Bwire, alisema marufuku hiyo ilitokana na kutokuwapo kwa askari wa kutosha kwa kuwa wako kwenye usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne, kidato cha pili na darasa la nne pamoja na kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia juu ya kutokea vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani.



















     Aidha,Kamanda huyo amesema sababu nyingine ni dalili za kuanza kampeni mapema za kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kabla ya kalenda ya kampeni kuanza.
    Vilevile,Kamanda huyo amebainisha kuwa sababu nyingine ni barua ya mkutano huo kutoweka wazi dhumuni la mkutano ikiwa ni kinyume cha kifungu cha 43(1)(b) cha Sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi sura 322 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
      Aidha,Msigwa akizungumza kuhusu kuzuiwa kwa mikutano yake amesema  hiyo ni kinyume cha sheria kwa kuwa Mbunge hutakiwa kutoa taarifa ili kuhakikisha usalama wa mikutano yake na si kuomba ruhusa kwa jeshi hilo.
   "Mimi ni mbunge na ile ndiyo kazi yangu. Sasa kazi yao ni kulinda mikutano yangu ili pasitokee vurugu na si kuzuia." Msigwa alisema.
    Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.