Header Ads

Header ADS

Waziri Kassim Majaliwa amwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM)

    Kassim Majaliwa Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania anatarajia kumwakilisha Rais Dkt.Magufuli leo Oktoba 26,katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko duniani utakaofanyika Baku, Azerbaijan.
    Ambapo dhumuni kubwa la mkutano huu ni kuitaji kujadili jinsi ya kutatua na kukabiliana na changamoto za kiuchumi,kisiasa na kijamii zinazokabili nchi wanachama wa NAM katika nyakati za sasa, pamoja na na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi wanachama wa umoja huo.
     Waziri Mkuu aliwasili nchini Azerbaijan jana (Ijumaa, Oktoba 25, 2019) na alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Bw. Ali Ahmadov pamoja na viongozi wengeine wa Serikali hiyo. Mapokezi hayo yalifanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heydar Aliyev.













      Ajenda za mkutano huo ni kupokea ripoti za mkutano wa maandalizi wa Mawaziri, kupokea ripoti ya mkutano wa maandalizi wa Maafisa Waandamizi, uchaguzi wa nchi zitakazokuwa wajumbe katika ofisi ya uratibu wa shughuli za NAM, New York kwa kipindi cha mwaka 2019-2022.
     Lakini pia,kufuatia ajenda hizo ambapo ajenda zingine katika mkutano huo ni kama vile kupokea ripoti za shughuli za umoja huo zilizotekelezwa chini ya Mwenyekiti wa NAM, Venezuela, mjadala mkuu, pamoja na kupitisha maandiko yatokanayo na mkutano.
   Aidha,Waziri Majaliwa katika mkutano huo ameshirikiana pamoja na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro na Balozi wa Tanzania Nchini Urusi ambale pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi.
   Hata hivyo,kabla ya mkutano huu Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Uchumi kati ya Urusi na Afrika (Russia - Africa Economic Forum) huko Sochi nchini Urusi ambapo baadae Mkutano wa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika uliofunguliwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

No comments

Powered by Blogger.