Header Ads

Header ADS

Nyumba 20 Mkoani Katavi zabomolewa na mvua kali.

     katika kijiji cha Kamsanga B, kilichopo Kata ya Mnyagala Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi zaidi ya nyumba 20 zabomoka kutokana na na mvua kali huku zingine zikiezuliwa mapaa,na kujeruhi watu watatu.
   Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon,akizungumzia tukio hilo ambapo amesema hadi sasa ni nyumba 20 zimeezuliwa na zingine 17 zimebomolewa.
    "Jana majira ya jioni mvua iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha na ikaezua mapaaa na tulifika kuangalia namna ya kuwanusulu ila nyumba ishirini mapaa yake yalikuwa yamedondoka na nyumba 17 ndiyo zilikuwa zimebomoka kabisa" amesema Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon.


  






     Salehe Mhando,mkuu wa Wilaya ya Tanganyika amewathili katika kijiji hicho ambapo ametoa pole kwa waathirika wa upepo huo,lakini hata hivo amesema  kuwa Serikali itaandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia.
    "Kwenye suala la ujenzi inabidi tuendelee kuelimishana ili tuweze kuweka vizuri, mfano nyumba ikiwa haijafungwa lenta ikipata misukosuko inabomoka" amesema Mkuu wa Wilaya.
    

No comments

Powered by Blogger.