Mamia ya Wasafiri wakwama enep la Mandela kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya Barabara.
Mamia ya abiria kutoka maeneo mbali mbali Nchini wamekwama katika Eneo la Korogwe na Handeni Mkoani Tanga ,tangu jana mchana sababu kubwa inayoeleza ni kutokana na Maji kupita juu ya Dalaja la Mandela na kusomba dalaja la handeni mkoani humo.
wakizungumza baadhi ya wasafiri akiwemo Jane Mathias na Juma kombo wamesema tangu jana saa 5 asubuhi wamekwama hapo kutokana na wingi wa maji ya Mvua zinazoendelea kunyesha mkoni humo.
"Tumefika hapa jana saa 5 asubuhi hadi muda huu (leo saa1 asubuhi) hatuoni uwezekano wa kuvuka," amesema Mathias.
Kombo ameiomba Serikali kuondoa adha hiyo kwa sababu kwa wiki mbili sasa daraja la Mandera limekuwa likijaa maji.
"Ni aibu barabara muhimu kama hii watu kukwama kutokana na daraja kujaa maji, kila siku wanajenga vivuko hawaimarishi barabara," amesema Mathias.
No comments
Post a Comment