Kocha Zahera aingia na mbinu nyingine Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema juzi na jana aliendelea kuifanyia marekebisho safu yake ya ulinzi kwa kuwaongezea mbinu walinzi wake na lengo ni kutokubali kuruhusu bao la ugenini.
Pia, amesema mabeki wa kati watacheza mkongwe Kelvin Yondani na Ali Ali wakati Yanga watakapowavaa Pyramids FC ya nchini Misri.
Aidha, Wataanza kucheza mabeki hao baada ya Mghana, Lamine Moro kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa pili wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika walipocheza dhidi ya Zesco United ya nchini Zambia.
Yanga, keshokutwa Jumapili itajitupa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kucheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids.
Zahera alisema kwa siku hizo mbili alikuwa na program maalum na mabeki wake hao wa kati na wa pembeni ambao ni Juma Abdul, Ally Mtoni na Issa Muharami ‘Marcelo’ ili kuhakikisha hawaruhusu krosi golini kwao.
Alisema kuwa siku hizo mbili zilitosha kwa mabeki wake kushika maelekezo hayo huku wakitarajia leo usiku kuzitazama video za wapinzani wao hotelini baada ya chakula cha usiku.
“Mimi kama kocha tayari nimewaona wapinzani wangu Pyramids kwa kupitia video na marafiki zangu wa karibu, ni wazuri kwenye mipira mirefu ya kushambulia kwa kushtukiza.
“Hivyo, ni lazima niwape mbinu mabeki wangu jinsi ya kucheza mipira hiyo na kikubwa tutakachokifanya ni kuzuia njia zao wanazozitumia katika kushambulia goli letu.
“Na mara nyingi wamekuwa wakitumia kushambulia kwa kupitia pembeni kwa kupiga krosi wakitumia miili yao kufunga kwa vichwa, hivyo tayari nimewapa mbinu mabeki wangu wa pembeni na nimewaambia wasiruhusu krosi golini kwetu,” alisema Zahera

No comments
Post a Comment