Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Tandahimba atoa agizo kwa watendaji kata na Vijiji.
Ahmada Suleiman ambae ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Tandahimba amewaagiza watendaji wa kata na vijiji kufuata mwongozo wa kanuni za uchaguzi katika kugawa fomu za wagombea katika maeneo yao
Amezungumza hayo katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba kwenye semina ya watendaji wa kata na vijiji.
"Tumieni kanuni za Uchaguzi katika kugawa fomu kwa wagombea haki itendeke kwa kila mgombea na baadhi ya watendaji msifanye kazi kwa mazoea kwakuwa kila Uchaguzi una mambo mapya,"alisema Suleiman
Ambapo amewataka wagombea wote kujitokeza kuchukua fomu kuanzia kesho tarehe 29 Oktoba katika maeneo yao ya kata na vijij.
Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira
No comments
Post a Comment