Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso ameagiza mkandarasi Ecar company limited aliyekuwa akiboresha mradi wa maji Lifua Manda wilayani ludewa mkoani Njombe kuondoshwa kazini Kufuatia kushindwa kukamilisha mradi huo kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipokabidhiwa mradi huo septemba 2017 mpaka sasa, na kusababisha wananchi kukabiliwa na adha kubwa ya upatikanaji wa maji.Naibu waziri ametoa agizo hilo wilayani Ludewa alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji. "Mradi huu ulitakiwa kutekelezwa tangu 2017 kwa muda wa miezi minne uwe umekamilika ili wananchi wapate maji sasa tangu 2017,2018,2019 leo tumebakisha miezi miwili kwenda 2020 lakini maji hakuna"alisema Juma Aweso."Lakini moja ya changamoto kubwa Sana ni kupeana kazi kishemeji shemeji kimjomba mjomba,Sasa mh. Rais dkt. John Pombe Magufuli alivyotuteua kuwa kwenye nafasi hizi pale Ikulu alituambia maneno machache sana kuwa nimekuteua kuwa kwenye nafasi ya wizara ya maji ambayo watanzania masikini waweze kupata maji na ndio maana nimekuja kujisalimisha mwenyewe"alisema Aweso. Aweso aliongeza kuwa"Kama kunatokea mtu wa kutukwamisha kwamisha basi hatutaelewana Mh. mbunge amesema huyu mkandarasi hana uwezo hata mimi nakiri hana uwezo lakini wataalamu wetu wametukosea, mkandarasi hana uwezo unampaje kazi kwa hiyo kikubwa hii tabia siitaki na huyu mkandarasi anayetekekeza huu mradi mara ya kwanza amepewa huu mradi ameshindwa,hatua ya pili maeshindwa mara ya tatu kam ama barua ya uchumba yaani wanabembelezana bembelezana sasa huyu bwana akatafute kazi ya kufanya"alisema. Pia Naibu Waziri huyo alisema anawachukia wakandarasi wababaishaji ambao wanawacheleweshea wananchi kupata maji ikiwa serikali inawekeza fedha nyingi kwa jambo hilo. Awali Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa alimwambia Naibu Waziri kuwa wananchi hao wamekua wakikumbana na changamoto nyingi wakati wa kutafuta maji hali inayopelekea wengine kupoteza maisha kutokana na kuliwa na mamba wakifuata maji mto Ruhuhu. Aidha wananchi wa kijiji cha Lihagule wilayani Ludewa mkoa wa Njombe walitoa kilio chao kwa naibu waziri wa maji Jumaa Aweso juu ya kuhatarisha maisha yao kwa kuuwawa na mamba wakienda kufuata maji mto Ruhuhu. Pia wamesema wanawake wanapata vipigo na kuachwa na wanaume zao kwa sababu ya kuamka usiku wa manane kwenda kufuata maji mlimani. Wananchi hao wametoa kilio hicho kufuatia mkandarasi Ecar anayetekekeza mradi wa maji Lifua_Manda unaogharimu takribani sh milioni 372 kushindwa kuukamilisha kwa wakati tangu mwaka alipopewa kazi hiyo 2017. Magnalena Haule ni mkazi wa Kijiji cha Lihagule alisema wanakwenda kuchota maji mto ruhuhu ambapo wakati mwengine wenzao hukamatwa na kuliwa na mamba. "Tukienda kuchota maji mto ruhuhu Kuna wenzetu wengine huwa wanaliwa na mamba,tunarudi kutoa taarifa kwamba kuna mwenzetu kachukuliwa na mamba wanaenda kumtafuta wakati mwingine wanamuona labda mamba kamla kichwa au miguu mwengine Unakuta aonekani kabisa"alisema Haule. Suzani Kayombo amesema kuwa wamekua wakiamka saa nne za usiku kwenda kufuata maji mlimani ambapo ukikuta foleni kubwa unalazimika kurudi asubuhi. "Kweli shida ya maji tunayo tunaamka usiku tunawaacha wanaume zetu ndani kwenda kutafuta maji na tunalala huko huko ni mlimani na maji yenyewe sio mazuri na wakati mwengine wanaume zetu hawatuelewi wanatupiga na wengine wameachwa"alisema. Mradi wa Lifua Manda una km 35 kutoka kilipo chanzo hadi shule ya sekondari Mandan ana unahudumia vijiji vya Lwilo,Lifua,Lihagule,Masasi na Manda sekondari ambao chanzo chake ni mto mchuchuma.
No comments
Post a Comment