Polisi Nchini Uganda wafuta tamasha la Bobi Wine
Maafisa wa polisi nchini Uganda wamefutilia mbali tamasha la mbunge wa Kyadondo mashariki Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine lililotarajiwa kufanyika karibu na mji mkuu wa Kampala.
Naibu inspekta jenerali wa polisi Asuman Mugyenyi anasema kwamba waandalizi wa tamasha hilo walishindwa kuweka usalama uliohitajika, kulingana na chombo cha habari cha Nile Post.
Alidai ukosefu wa mipango ya matibabu, udhibiti wa idadi ya watu na usalama kama baadhi ya maswala yaliowashinikiza kulifuta tamasha hilo.Tamasha hilo lilikuwa liingiliane na siku ya Uhuru inayoadhimishwa Jumatano katika wilaya ya mashariki ya Siroko.
Mgombea huyo wa urais ni mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni na anajionyesha kuwa mpiganiaji wa masikini.
Aliambia waandishi wiki iliopita kwamba tamasha hilo litaendelea kama lilivyopangwa licha ya maafisa wa polisi kushindwa kujibu barua ilioandikwa ikiomba kuandaa tamasha hilo.
Kufutwa kwa tamasha hilo kunajiri baada ya marufuku ya serikali kuhusu uvaaji wa kofia ya rangi nyekundu na raia, nembo ambayo Bobi Wine amekuwa akiitumia katika vuguvugu lake la nguvu za raia.
Chini ya sheria mpya iliotangazwa mwezi uliopita, kofi hiyo kwa jina Red Beret inafaa kuvaliwa na jeshi la - UPDF.
Mwanamuziki huyo aliyebadilika na kuwa mwanasiasa amechapisha picha katika mtandao wake wa twitter akionyesha maafoisa wa polisi walioizunguka nyumba yake , mbali na vizuizi vilivyowekwa katika barabara iliokuwa ikielekea katika nyumba yake.
Pia alidai kwamba maafisa wa polisi walizunguka mali ya ya One Love Beach Busabala , ambalo ndio eneo la Tamasha hilo.
No comments
Post a Comment