Header Ads

Header ADS

Mfumuko wa Bei wa Taifa wapungua

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2019.
   Mkuruguenzi wa Takwimu za jamii na Sensa za watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimi Bi.Ruth Minja ameyasema hayo wakati akitangaza Mfumuko wa Bei jana Jijini Dodoma.
“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha  Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.













Aidha amesema kuwa bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba  ni pamoja na Mafuta ya Taa  asilimia 1.0,Petrol asilimia 3.3,Majiko ya gesi asilimia 1.5,dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2,mauta ya nywele asilimia 1.3.
 Pia Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.
   Bi.Minja akizungumzia Nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa mfumuko wa bei Nchini Kenya umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosto 2019.
   Kwa upande wa Nchi za Uganda Mfumuko wa Bei Kwa Mwaka unaoishia Mwezi Septemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9  kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti 2019.

   









No comments

Powered by Blogger.